Global Publishers
March 20, 2026
0 Comments
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi kumi na moja (11) baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Waombaji wote wanahimizwa kuwasilisha maombi yao kwa kuzingatia sifa na masharti yaliyobainishwa hapa chini:
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI >>>HALMASHAURI YA WILAYA YA BARIADI 19-03-2026
1. Dereva Daraja la II – Nafasi 7
Majukumu
-
Kukagua gari kabla na baada ya safari
-
Kusafirisha watumishi kwenye shughuli za kikazi
-
Kufanya matengenezo madogo ya gari
-
Kusambaza na kukusanya nyaraka
-
Kujaza daftari la safari
-
Kusafisha gari
-
Kazi nyingine atakazopangiwa
Sifa za Mwombaji
Mshahara
2. Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Nafasi 4
Majukumu
-
Kuorodhesha barua zinazoingia na kutoka
-
Kusambaza na kupokea mafaili
-
Kufuatilia mzunguko wa majalada
-
Kupanga na kuhifadhi nyaraka
-
Kuweka kumbukumbu kwenye masjala
-
Kazi nyingine atakazopangiwa
Sifa za Mwombaji
Mshahara
Masharti ya Jumla
-
Raia wa Tanzania
-
Umri: miaka 18 – 45
-
Wenye ulemavu wanahamasishwa kuomba
-
Wasio na vyeti halali (testimonials/results slips) hawatakubaliwa
-
Maombi yaambatane na CV, vyeti, na wadhamini 3
-
Waombaji wa umma wapitishe maombi kupitia kwa waajiri wao
-
Vyeti vya nje ya nchi lazima vihakikiwe (TCU/NECTA/NACTE)
-
Wastaafu wa umma wanahitaji kibali maalum
-
Maombi yawe kupitia mfumo wa ajira: https://portal.ajira.go.tz
-
Mwisho wa kutuma maombi: 31/03/2026