KATIKA mwendelezo wa kuunga mkono jamii na kukuza uchumi wa watu wa hali za chini, Meridianbet imeandika historia nyingine kwa kugusa maisha ya kina mama wajasiriamali maarufu kama Mama Lishe. Safari hii, kampuni hiyo imefika moja kwa moja mtaani na kugawa aproni kwa kina mama wanaouza vyakula, ikiwa ni ishara ya kuthamini kazi yao kubwa.
Tukio hilo lilifanyika katika eneo maarufu la Coco Beach, Oyster Bay, mahali penye mkusanyiko mkubwa wa Mama Lishe wanaohudumia wakazi wa jiji la Dar es Salaam na wageni wanaotembelea ufukwe huo. Mandhari ilikuwa ya kuvutia, furaha na shukrani zikitawala huku kina mama wakipokea msaada huo muhimu kwa kazi zao za kila siku.
Vilevile, Michezo mingi zaidi ya kubashiri inaendelea kupatikana ndani ya Meridianbet ikiwa na ODDS kubwa na machaguo mengi zaidi. Kushiriki ni vyepesi kupitia tovuti ya MERIDIANBET au kwa kupiga *149*10#.
Mwakilishi wa Meridianbet, Nancy Ingram, alieleza kuwa lengo kuu la kampuni ni kuendelea kusapoti wajasiriamali wadogo, hasa wanawake, ambao mara nyingi ndiyo uti wa mgongo wa jamii na pia ni sehemu muhimu ya wateja wao. Alisisitiza kuwa Meridianbet inaamini katika kurudisha kwa jamii na kusaidia kukuza kipato kwa watu wa kawaida ili kuimarisha maisha yao.
Kwa upande wao, Mama Lishe hawakusita kuonyesha furaha yao kubwa na kutoa shukrani za dhati kwa Meridianbet kwa kuwajali na kuwathamini. Walisema msaada huo sio tu unawasaidia katika kazi zao bali pia unawapa motisha ya kuendelea kupambana na kujikwamua kiuchumi.
Meridianbet inaendelea kuthibitisha kuwa sio tu kinara wa burudani ya michezo ya kubashiri, bali pia ni mshirika wa kweli wa jamii. Hii ni ishara kwamba pamoja na kushinda kwenye michezo, unaweza pia kushinda kwenye maisha kupitia fursa na msaada unaotolewa na Meridianbet, hapa ushindi ni zaidi ya mkeka kutiki, ni maisha halisi.


