VIJANA WAASWA KUSOMA MIKATABA KABLA YA KUKUBALI HUDUMA

Afisa Mlinda Mlaji Mwandamizi FCC Bi.Magdalena Hall,akitoa elimu kuhusu masuala ya kumlinda mlaji na mikataba ya walaji kwa wanafunzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi VETA Kibaha ,ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.

….

KATIKA harakati za kuimarisha uelewa wa haki za walaji nchini, Tume ya Ushindani (FCC) leo Machi 19, 2026 imetoa elimu kwa wanachuo wa Chuo Cha Ufundi Stadi VETA Kibaha kuhusu masuala ya kumlinda mlaji na mikataba ya walaji, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.

Elimu hiyo ilitolewa na FCC kwa lengo la kuwajengea uelewa wanachuo kuhusu haki zao wanapokuwa wanatumia bidhaa na huduma mbalimbali. Wanachuo walipata nafasi ya kujifunza mambo muhimu ambayo mara nyingi huyapuuzia katika maisha yao ya kila siku.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo,Afisa Mlinda Mlaji Mwandamizi FCC Bi.Magdalena Hall,amewaeleza wanachuo kuwa wengi wao huingia katika mikataba bila kusoma masharti yake, hali inayoweza kusababisha hasara au kunyimwa haki zao bila wao kutambua.

Amefafanua kuwa mikataba mingi hasa ya huduma za simu, mikopo na manunuzi ya mtandaoni huwa na vifungu vinavyohitaji umakini mkubwa kabla ya kukubaliwa. Hivyo aliwataka wanachuo kujenga utamaduni wa kusoma na kuelewa kila wanachosaini.

Aidha, amesema kuwa mlaji ana haki ya kupata bidhaa bora, taarifa sahihi na huduma stahiki. Pale haki hizo zinapokiukwa, mlaji anatakiwa kuchukua hatua za kisheria au kuripoti kwa mamlaka husika.

“FCC imesisitiza kuwa elimu hii ni endelevu na inalenga kuwafikia makundi mbalimbali ya jamii ili kujenga taifa lenye walaji wenye uelewa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi.”amesema Bi.Hall

Kwa ujumla, mafunzo hayo yamewajengea wanachuo uelewa mkubwa na kuwahamasisha kuwa mabalozi wa haki za walaji, huku yakichangia mafanikio ya maadhimisho ya Maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.

Afisa Mlinda Mlaji Mwandamizi FCC Bi.Magdalena Hall,akitoa elimu kuhusu masuala ya kumlinda mlaji na mikataba ya walaji kwa wanafunzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi VETA Kibaha ,ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.

Afisa Mlinda Mlaji Mwandamizi FCC Bi.Magdalena Hall,akitoa elimu kuhusu masuala ya kumlinda mlaji na mikataba ya walaji kwa wanafunzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi VETA Kibaha ,ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.

Afisa Mlinda Mlaji Mwandamizi FCC Bi.Magdalena Hall,akitoa elimu kuhusu masuala ya kumlinda mlaji na mikataba ya walaji kwa wanafunzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi VETA Kibaha ,ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.

Sehemu ya wanafunzi wa wanafunzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi VETA Kibaha wakisikiliza mada mbalimbali wakati wakipata elimu kuhusiana na masuala ya kumlinda mlaji na mikataba ya walaji kwa ,ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.

Wanafunzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi VETA Kibaha wakiuliza maswali mbalimbali kuhusu namna ya kutofautisha mikataba halisi na feki mara baada ya kupatiwa elimu na FCC ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani.

Afisa Mlinda Mlaji Mwandamizi FCC Bi.Magdalena Hall,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi VETA Kibaha mara baada ya kuwapatia elimu kuhusu masuala ya kumlinda mlaji na mikataba ya walaji kwa ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani 2026.