Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya wakulima na Wanufaika wa mradi wa mashamba ya Serikali ya Jenga kesho iliyobora(BBT)wapatao 300 katika Kijiji cha Mlazo kata Ndogowe Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wamepatiwa Semina ya kufahamu changamoto ya Afya ya Akili,Afya ya Uzazi na namna ya kujinginga na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya Ngono.
Msomaji Lusinde na Sharifa Athuman Isaka miongoni kwa vijana na wananchi wa Ndogowe wamesema kuwa Semina hiyo imewajengea Imani,matumaini,uvumilivu na uhakikika wa upatikanaji wa mazao kupitia shughuli zao za kilimo biashara
Wameongeza kwa kusema kuwa hapo awali walikuwa hawana uelewa kuhusu chanagamoto ya Afya ya Akili na Afya ya Uzazi ambapo wameahidi kutumia elimu waliyoipata kupitia semina hiyo kuongeza nguvu katika shughuli zao za kilimo biashara
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji Cha Mlazo Mahawi Makasi amesema kuwa katika eneo hilo hawajawahi kupatiwa semina ya namna hiyo hivyo Serikali kupitia BBT imefanya jambo jema ambapo pia ameomba Semina hiyo iwe endelevu
Naye Afisa anayeshughulikia Masuala ya kijinsia,Jamii na Maendele kutoka BBT Neema Urasa amesema kuwa kutokana na vijana hao kukaa shambani kwa muda mrefu kwa ajili ya shughuli ya kilimo biashara wameona ni vyema kukaa nao na kuzungumza nao masuala ya changamoto ya Afya ya Akili,masuala ya Afya ya uzazi na kujifunza na namna ya kujikinga na magongwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono.

.jpeg)
.jpeg)

