Rais Hussein Ali Mwinyi Ashiriki Swala ya Eid al-Fitr Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Eid al-Fitr iliyosaliwa leo, tarehe 21 Machi 2026, katika Msikiti wa Jamiu Zanjibar, Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Waumini wa dini ya Kiislamu wanasherehekea Sikukuu ya Eid al-Fitr baada ya kukamilika kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ibada hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali, viongozi wa dini pamoja na waumini mbalimbali wa dini ya Kiislamu.