Global Publishers
March 21, 2026
0 Comments
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale ametangaza rasmi nafasi za kazi 31 kwa Watanzania wenye sifa, baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Tangazo hilo linahusisha nafasi katika kada tatu tofauti ambazo ni Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II, Dereva Daraja la II, na Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II.
NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA LIWALE 17-03-2026
Kwa mujibu wa tangazo hilo, waombaji wote wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia mfumo wa kielektroniki wa ajira kupitia Recruitment Portal (https://portal.ajira.go.tz/) kabla ya tarehe ya mwisho ya maombi iliyowekwa kuwa 30 Machi 2026.
1. Nafasi za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II (11)
Waombaji wanapaswa kuwa na:
-
Kidato cha Nne
-
Stashahada (Diploma) ya Uhazili au NTA Level 6
-
Uwezo wa kuandika kwa kasi (80 w.p.m) kwa Kiswahili na Kiingereza
-
Ujuzi wa programu za kompyuta kama Word, Excel, PowerPoint, Email na Internet
Majukumu yake ni pamoja na kuchapa nyaraka, kupokea wageni, kutunza kumbukumbu, na kuandaa vikao mbalimbali.
2. Nafasi za Dereva Daraja la II (13)
Sifa kuu ni:
-
Kidato cha Nne
-
Leseni ya udereva Daraja C au E
-
Mafunzo ya udereva kutoka taasisi inayotambuliwa (kama VETA)
-
Uzoefu wa kuendesha gari bila ajali kwa angalau mwaka mmoja
Majukumu yake ni kuendesha magari ya serikali, kukagua magari, kutunza kumbukumbu za safari na kufanya matengenezo madogo.
3. Nafasi za Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II (7)
Sifa zinazohitajika ni:
Majukumu yake ni pamoja na kusajili barua zinazoingia na kutoka, kusambaza majalada, kufuatilia mzunguko wa nyaraka na kuhifadhi kumbukumbu.
Masharti ya Jumla kwa Waombaji
-
Awe raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 18 hadi 45
-
Aambatanishe vyeti vilivyothibitishwa na mwanasheria
-
Awasilishe CV yenye wadhamini watatu
-
Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kuainisha hali zao
-
Waombaji walioko kazini Serikalini wapitishe maombi kupitia waajiri wao
-
Vyeti vya “statement of results” havitakubaliwa
-
Waombaji waliosomea nje wahakikishe vyeti vyao vimeidhinishwa na mamlaka husika
Tarehe ya Mwisho
📅 30 Machi 2026