Global Publishers
March 22, 2026
0 Comments
Rais wa Marekani, Donald J. Trump, ametuma ujumbe mkali akiilenga Iran kuhusu hali ya usalama katika eneo la Strait of Hormuz.
Kupitia ujumbe uliosambaa mtandaoni, Trump ameonya kuwa Iran inapaswa kufungua njia hiyo muhimu ya kimataifa bila vitisho ndani ya muda maalum wa saa 48, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa usalama wa biashara na usafirishaji wa mafuta duniani.
Amesema endapo Iran haitatekeleza hilo ndani ya muda huo, basi Marekani iko tayari kuchukua hatua kali za kijeshi. Aidha, ameongeza kuwa hatua hizo zinaweza kuanza kwa kulenga miundombinu muhimu ya nishati, ikiwemo mitambo mikubwa ya uzalishaji wa umeme.
Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa kimataifa, huku wachambuzi wengi wakieleza kuwa ni ishara ya kuongezeka kwa mvutano kati ya United States na Iran, hali inayoweza kuathiri usalama wa eneo la Mashariki ya Kati pamoja na uchumi wa dunia.
Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na upande wa Iran kujibu kauli hiyo, huku eneo la Strait of Hormuz likiendelea kubaki kitovu muhimu cha uchumi wa dunia, hasa katika usafirishaji wa mafuta.
