THPS YAKABIDHI KLINIKI YA MAT SHINYANGA KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

 

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo (wa pili kushoto), akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Yudas Ndungile, wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana akifuatiwa na Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia. Picha na Kadama Malunde 

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo (katikati), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medication-Assisted Treatment – MAT) lililojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026.

Muonekano wa Jengo la Kliniki ya MAT lililojengwa na Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akiwa kwenye Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) limekabidhi rasmi Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medically-Assisted Treatment – MAT) katika Manispaa ya Shinyanga kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatua ambayo inaimarisha juhudi za kupambana na changamoto ya matumizi ya dawa za kulevya nchini.

Kliniki hiyo, iliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB wenye thamani ya shilingi milioni 145, ni matokeo ya ushirikiano kati ya THPS, CRDB, Wizara ya Afya, DCEA, na Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, ikizingatia viwango vya kitaifa vya huduma za afya.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Machi 22, 2026 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amesema kuwa kliniki hiyo ni nyenzo muhimu katika kupunguza madhara ya uraibu wa dawa za kulevya.

Aidha, amewapongeza wadau waliofanikisha ujenzi huo, likiwemo Shirika la THPS na Benki ya CRDB, akieleza kuwa mchango wa sekta binafsi unaonyesha namna taasisi za kifedha zinavyoweza kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto za kijamii.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo.

“Napenda kuipongeza na kuishukuru THPS kwa jitihada zao za kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya. Pia naishukuru Benki ya CRDB kwa msaada wao mkubwa. Nawahimiza wananchi, hususan vijana walioathirika, kutumia huduma hizi ili kwa pamoja tulinde afya na mustakabali wa jamii zetu,” amesema Lyimo.

Ameongeza kuwa uraibu wa dawa za kulevya ni changamoto kubwa inayogusa afya, uchumi, na ustawi wa jamii, na kwamba mapambano dhidi ya tatizo hilo yanahitaji ushirikiano wa wadau wote kuanzia familia hadi ngazi ya Taifa.

 Lyimo amesema huduma za tiba ya uraibu (MAT) zimekuwa nyenzo muhimu kupunguza madhara ya dawa za kulevya kwa kusaidia waraibu kupunguza utegemezi, kudhibiti maambukizi ya magonjwa kama VVU/UKIMWI, na kupunguza vitendo vya uhalifu na vifo vinavyotokana na matumizi ya dawa hizo.

Kamishna Lyimo ameongeza kuwa kliniki hii ya Shinyanga ni ya 22 nchini, hatua inayothibitisha dhamira ya Serikali ya kupanua huduma za MAT ili kuwafikia wananchi wengi zaidi wanaohitaji msaada wa matibabu.

 Pia amesisitiza umuhimu wa jamii kuacha unyanyapaa dhidi ya waraibu wa dawa za kulevya na badala yake kuwasaidia kupata matibabu, huku akihimiza malezi bora kwa vijana ili kuwalinda dhidi ya kujiingiza kwenye uraibu.

Ameeleza kuwa baada ya uzinduzi, wataalamu kutoka DCEA kwa kushirikiana na Wizara ya Afya watatoa mafunzo maalum kwa watumishi wa afya ili kuhakikisha huduma zinaanza kutolewa kwa ufanisi na kwa kuzingatia viwango vya kitaaluma. 

“Kupitia tiba ya Methadone na huduma jumuishi, wapokeaji watapewa uwezo wa kudhibiti uraibu, kupunguza hatari za kiafya, na kurejea katika maisha ya kawaida ya kijamii,” amesema Lyimo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia, amesema kabla ya kuanzishwa kwa kliniki hiyo, waraibu wengi wa dawa za kulevya kutoka Shinyanga walilazimika kusafiri hadi Mkoa wa Mwanza kupata matibabu, hali iliyosababisha baadhi yao kushindwa kufikia huduma hizo kwa urahisi.

Mkurugenzi wa THPS Dkt. Redempta Mbatia (katikati), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya MAT Shinyanga.

Dkt. Redempta ameeleza kuwa ndipo walipoamua kuomba ufadhili kutoka CRDB Bank ili kujenga kituo hicho, ambacho sasa ni cha kwanza cha aina yake katika Mkoa wa Shinyanga.

“Tunajivunia kuona jitihada hii muhimu ikifanikiwa. Naishukuru Benki ya CRDB kwa msaada wao na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake endelevu. Huu ni mfano mzuri wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi katika kuimarisha upatikanaji, usawa na ubora wa huduma za afya, sambamba na ajenda ya Uhakika wa Afya kwa Wote,” amesema Dkt. Redempta.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Abdulmajid M. Nsekela, amesema benki hiyo ina utaratibu wa kutenga asilimia moja ya faida baada ya kodi (VAT) kwa ajili ya kurejesha kwa jamii kupitia miradi ya afya, elimu, mazingira na maeneo mengine ya kijamii.

Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.

“Benki ya CRDB inathamini ushirikiano wake na THPS pamoja na Serikali ya Tanzania na zaidi niwapongeza THPS ambao walileta kwetu wazo hili na sisi tukafanya ufadhili huu. Kusaidia ujenzi wa kliniki hii ni kielelezo cha dhamira yetu ya kuboresha ustawi wa jamii tunamofanya biashara na kuifanya benki ya CRDB kuwekeza kwa jamii badala ya kufanya biashara pekee. Tukiwa kama benki kiongozi nchini Tanzania, tutaendelea kuunga mkono programu zenye matokeo chanya na endelevu kwa jamii,” amesema Wagana.

“Huu ni mwendelezo na tunaahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kusaidia miradi ya serikali. Tunaamini katika mashirikiano ya Serikali na sekta binafsi ndo chachu ya mafanikio katika maendeleo. Mwisho tunawaomba wadau wote – wafanyakazi, wafanyabiashara, wastaafu, vijana, na makundi yote – kuendelea kutumia huduma za CRDB nchini Tanzania ili asilimia moja baada ya kodi iweze kuongezeka na kusaidia maeneo mbalimbali yenye uhitaji”,ameongeza Wagana.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, amesema tayari maandalizi muhimu yamekamilika ikiwemo upatikanaji wa watumishi wa afya, samani za kliniki pamoja na maboresho ya mazingira ya kituo hicho ili kuhakikisha huduma zinaanza kutolewa kwa ufanisi.

Aidha, ameomba wadau kuendelea kuunga mkono kituo hicho kwa kukiwezesha kupata vifaa muhimu zaidi ikiwemo mashine za kupima kiwango cha matumizi ya dawa (meter measure) ili kusaidia kupanga dozi sahihi kwa wagonjwa kulingana na kiwango cha uathirika.

Kuhusu THPS

Tanzania Health Promotion Support (THPS) ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa nchini Tanzania na kusajiliwa chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002, lenye dhamira ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa Watanzania wote.

Tangu mwaka 2011, THPS imekuwa ikishirikiana wa Serikali ya Tanzania katika kuimarisha mifumo ya afya na jamii—kupambana na magonjwa ya kuambukiza na yale yamlipuko, magonjwa yasiyoambukiza, afya ya uzazi, mama, mtoto mchanga, vijana na watoto, pamoja na kuondoa vikwazo vya kimuundo katika upatikanaji wa huduma za afya.

Kupitia ushirikiano wa kimkakati na mbinu zinazotokana na utafiti wa kisayansi, THPS inaendelea kuchangia katika maboresho ya afya endelevu na kushirikiana katika kuandaa na kutathmini afua za afya ya umma.

Kuhusu Huduma za tiba kwa waraibu (MAT)

Huduma za MAT ni huduma za afya zinayolenga watu wanaotumia dawa za kulevya, hasa wanaotegemea dawa za kulevya aina ya opioidi kama heroini. 

Huduma hii hutumia mchanganyiko wa dawa maalum, ushauri nasaha na tiba ya kisaikolojia ili kusaidia watu kuacha au kupunguza matumizi ya dawa hatarishi na kuimarisha afya zao.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo (wa pili kushoto), akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medication-Assisted Treatment – MAT) lililojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, pamoja na Mkurugenzi wa Tanzania Health Promotion Support, Redempta Mbatia. 

Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia (wa pili kulia) akizungumza wakati Uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026. Wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile, akifuatiwa na Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, wa kwanza kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kliniki ya MAT iliyojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. 

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akipata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa katika Kliniki ya MAT kutoka kwa mtaalamu wa afya.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo (katikati), akipata maelezo kuhusu Huduma zinazotolewa katika Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akizungumza wakati akitembelea Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia akielezea kuhusu Huduma zinazotolewa katika Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Muonekano wa Jengo la Kliniki ya MAT lililojengwa na Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (Medication-Assisted Treatment – MAT) lililojengwa na Shirika la Tanzania Health Promotion Support (THPS) kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Machi 22, 2026.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akizungumza wakati akizindua Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jengo la Kliniki ya Huduma za Tiba kwa Waraibu wa Dawa za Kulevya (MAT) lililojengwa na THPS kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akizungumza kuhusu umuhimu wa huduma za MAT katika kupambana na uraibu wa dawa za kulevya.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Luzila John akielezea namna huduma zitakavyotolewa.

Kamishna wa Kinga na Tiba wa DCEA, Dkt. Peter Patrick Mfisi akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

Mnufaika wa huduma za MAT, Ibrahim Seif akieleza jinsi alivyofanikiwa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya baada ya miaka 10.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akisalimiana na Mkurugenzi wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akisalimiana na Meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akisalimiana na Kamishna wa Kinga na Tiba wa DCEA, Dkt. Peter Patrick Mfisi