MADAKTARI 30 KUTOKA CHINA KUTIBU BURE UBUNGO DAR ES SALAAM

*****

Zaidi ya madaktari bingwa 30 kutoka China na Tanzania wanatarajiwa kuweka historia mpya ya huduma za afya jijini Dar es Salaam, kwa kuanzisha kambi maalum ya matibabu ya bure itakayodumu kwa siku mbili mfululizo, Machi 28 na 29, mwaka huu.

Kambi hiyo itafanyika katika viwanja vya East Africa Commercial Logistics Centre (EACLC), ikiwa ni jitihada za pamoja za wadau wa afya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora bila gharama yoyote.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, amewataka wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na fursa hiyo adhimu ya kupimwa na kutibiwa bure.

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando akimzungumza Jiji Dar es salaam.

Msando alisisitiza kuwa huduma hizo zitatolewa kwa wananchi wote bila ubaguzi, akiwahimiza wazazi na walezi kuhakikisha wanawaleta watoto wao pamoja na watu wenye changamoto mbalimbali za kiafya.

Kwa upande wake, Afisa Uhusiano wa EACLC, Linda Mtui, alisema kambi hiyo itatoa huduma mbalimbali ikiwemo vipimo vya shinikizo la damu, kisukari, macho, masikio, koo pamoja na ushauri wa kitaalamu wa afya.

Afisa Uhusiano wa EACLC, Linda Mtui, kulia niMkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando.

Aliongeza kuwa huduma za afya kwa wanawake na watoto pia zitapewa kipaumbele, hatua inayolenga kugusa makundi nyeti ambayo mara nyingi hukosa huduma za uhakika kwa wakati.

Naye daktari bingwa kutoka China, Bao Zegtao, alisema lengo la ujio wao ni kusaidia jamii zenye uhitaji mkubwa wa huduma za afya, akibainisha kuwa wamekuwa wakifanya huduma kama hizo katika nchi mbalimbali duniani.

Daktari bingwa kutoka China, Bao Zegtao kushoto niĀ  Afisa Uhusiano wa EACLC, Linda Mtui.

Picha ya pamoja Mkuu Wa wilaya na Viongozi wa EACLC na madaktaria watakaotoa Huduma za afya jijini Dar es Salaam, kwa kuanzisha kambi maalum ya matibabu ya bure itakayodumu kwa siku mbili mfululizo, Machi 28 na 29, mwaka huu.