Video: Polisi Wakamata Mgambo Watatu kwa Mauaji ya Kijana Bugando

Global Publishers
March 23, 2026
0 Comments

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewakamata askari mgambo watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kijana Rashid Masunga Nyandonga (31), mkazi wa Bugando wilayani Nyamagana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Machi 22, 2026, tukio hilo lilitokea Machi 20, 2026 majira ya saa 12:45 jioni katika mtaa wa Mission, eneo la Sahara, kata ya Pamba.

Inadaiwa kuwa askari mgambo hao walimtuhumu marehemu kuwa anauza dawa za kulevya aina ya mirungi kabla ya kuanza kumfukuza.

Katika tukio hilo, marehemu alikimbia akijaribu kukwepa kukamatwa, lakini askari hao walimkamata baada ya kumfukuza na kumpiga.

Watuhumiwa waliokamatwa ni Zongoli Makongoro (38), Genge Chacha Mwita (45), na Ibrahim Chacha Mwita (25).

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea huku watuhumiwa hao wakiendelea kushikiliwa.