Global Publishers
March 24, 2026
0 Comments
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, leo Machi 24, 2026 amekagua ukumbi wa Bunge ulioboreshwa kwa kuwekewa mfumo wa kisasa wa sauti, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa 3 wa Bunge la 13.
Mkutano huo maalum unatarajiwa kuanza Machi 31, 2026, ukiwa na lengo la kujadili na kupitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Katika hatua nyingine, Spika Zungu ameongoza kikao cha Tume ya Watumishi wa Bunge kilichojadili na kupitisha makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Bunge kwa mwaka huo wa fedha.
Maandalizi hayo yanaashiria utayari wa Bunge kuendesha vikao vyake kwa ufanisi zaidi, huku maboresho ya miundombinu yakilenga kuongeza ubora wa mijadala na mawasiliano ndani ya ukumbi huo muhimu wa kitaifa.


