Global Publishers
March 24, 2026
0 Comments
Klabu ya Yanga, imetangaza kumrejesha kocha Abdihamid Moalin kuwa kocha Msaidizi chini ya Kocha Mkuu Pedro Gonçalves hatua ambayo klabu hiyo imeeleza kuwa imalenga kutatua changamoto ya kiufundi klabu hiyo inayopelekea kupata wakati mgumu kupata matokeo mazuri na kucheza vizuri.
Taarifa ya Machi 23, 2026 iliyotolewa na klabu hiyo na klabu hiyo baada ya kikao cha kufanya tathimini ya timu hiyo baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu imeeleza kuwa uongozi WA klabu umegundua uwepo wa changamoto ya kiufundi inayoifanya Timu icheze aina tofauti ya uchezaji (style of play) ile ambayo imezoelekea na kuendana na wachezaji walio ndani ya kikosi.
Kocha Moalin amewahi kuhudumu Young Africans Sc kama Mkurugenzi wa Ufundi na Kocha Msaidizi katika vipindi tofauti chini ya Kocha Sead Ramovic na Miloud Hamdi na kupata mafanikio makubwa ya kushinda Kombe la Ligi Kuu 2024/2025, Kombe la Shirikisho la CRDB 2025na Kombe la Muungano 2025.
Yanga SC imewaahidi Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Klabu hiyo kuwa, Timu hiyo itarudi mzunguko wa pili ikiwa imara na nguvu kubwa kuelekea kutimiza malengo ya klabu kwa Msimu wa 2025/26, kwa kushinda Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho la CRDB.
