RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AZIDI KUNG’AA KIMATAIFA

………

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU), Mahamoud Ali Youssouf amemteua Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mwakilishi maalum wa ngazi ya juu anayesimamia na kuratibu masuala ya amani na usalama katika eneo la Pembe ya Afrika.

Aidha, Rais Kikwete atasimamia pia ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi, migogoro na diplomasia ya kimataifa ikiwamo masuala ya Bahari ya Shamu kama usafirishaji na usalama wa baharini.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Tume hiyo kwa vyombo vya habari, Nuur Mohamud Sheekh imesema kuwa mwenyekiti wa Tume hiyo anaimani na utendaji kazi wa Rais mstaafu Kikwete na anamini atasaidia juhudi za kutafuta amani katika eneo hilo.

Majukumu mengine ni pamoja na kuwakilisha taasisi/nchi kimataifa katika eneo hilo, kutatua migogoro kati ya nchi za eneo hilo, kusimamia miradi ya maendeleo na ushirikiano na kushauri viongozi wa juu kuhusu sera za eneo hilo.

Rais mstaafu Kikwete anakwenda kuwa balozi maalum wa ngazi ya juu anayeshughulikia siasa, usalama na ushirikiano katika eneo la Pembe ya Afrika.