Mkurugenzi wa Program ya Rasimisha Leah Kalunde akizungumz katika katika hafla maalum ya kusheherekea siku ya wanawake hodari iliyowakutanisha wanawake wanaofanya biashara mbalimbali ambayo imefanyika Tae 24/3/2026 jijini Dar es salaamMeneja mradi wa Program ya Rasimisha Caroline Andrew akiwasilisha taarifa maalum kuhusu Rasimisha katika hafla maalum ya kusheherekea siku ya wanawake hodari iliyowakutanisha wanawake wanaofanya biashara mbalimbali ambayo imefanyika Tae 24/3/2026 jijini Dar es salaam

Mkurugenzi wa Kairosi Anna Luvanda akizungumza katika katika hafla maalum ya kusheherekea siku ya wanawake hodari iliyowakutanisha wanawake wanaofanya biashara mbalimbali ambayo imefanyika Tae 24/3/2026 jijini Dar es salaam
Baadhi ya wanawake walioshiriki katika katika hafla maalum ya kusheherekea siku ya wanawake hodari iliyowakutanisha wanawake wanaofanya biashara mbalimbali ambayo imefanyika Tae 24/3/2026 jijini Dar es salaam (Picha zote na Mussa Khalid)
……………..
Wanawake wajasiriamali nchini wametakiwa kutumia fursa ya uwepo wa mpango wa Rasimisha ili kuwawezesha kufanya biashara endelevu zenye kuleta matokeo chanya.
Akizungumza jijini Dar es salaam katika hafla maalum ya kusheherekea siku ya wanawake hodari iliyowakutanisha wanawake wanaofanyabiashara biashara mbalimbali,Mkurugenzi wa Rasimisha Program Leah Kalunde amesema kuwa lengo la mpango huo ni kuhakikisha linabadilisha biashara zisizo rasmi kuwa zilizo na muundo na zinazoweza kukua na kuvutia uwekezaji.
Amesema kuwa rasimisha ni sauti ya mtoto wa kitanzania ambaye amekulia kwenye mazingira ya kawaida ya wazazi kuapmbana kuhakikisha watoto wanapata maisha bora.
Awali akiwasilisha taarifa maalum kuhusu Rasimisha,Meneja mradi wa mradi huo Caroline Andrew amesema kuwa kupitia mfumo huo wafanyabiashara wataweza kuona uhalisia wa biashara zao ikiwemo kujenga kumbukumbu za kifedha zinazoaminika.
Kwa upande wao Mratibu wa Malipo Mtandao Ritha Mongi amesema lengo lao ni kuwawezesha wafanyabiashara kuongeza thamani za biashara zao huku,Mkurugenzi wa Kairosi Anna Luvanda amesema elimu imekuwa ikiwafikia kupitia vikundi vya kusaidiana kwenye shida na raha.
Hata ivyo imeelezwa pia mpango huo utahakikisha hakuna mwanamkwe anayeachwa nyuma kwani itasaidia kugeuza uwezo wa mwanamke kuwa nguvu ya kiuchumi inayoonekana na kuthaminiwa.













