Kwa mujibu wa tathmini ya IFC ya mwaka 2025, taasisi hiyo imewekeza takribani dola milioni 197.4 katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026, kupitia mikopo ya muda mfupi iliyolenga kuchochea shughuli za sekta binafsi.
Kiasi cha uwekezaji wa IFC nchini Tanzania kimefikia dola milioni 315.9, ambapo asilimia 74 imeelekezwa katika sekta ya huduma za kifedha na asilimia 26 katika viwanda, kilimo-biashara, na huduma nyingine.
IFC pia inaunga mkono utekelezaji wa Mradi wa Usafiri wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT) jijini Dar es Salaam kupitia huduma za ushauri wa PPP, pamoja na kutekeleza Mpango wa Kitaifa wa Jinsia (Gender Program) wenye thamani ya dola milioni 6.3 hadi mwaka 2028, unaolenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika shughuli za kibiashara.
Kikao hicho kilihudhuriwa na maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati, Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), pamoja na wawakilishi wa IFC.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiongoza kikao chake na ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) Kanda ya Afrika Mashariki, ukiongozwa na Mkurugenzi wake, Bi. Mary Porter Peschka, baada ya kukutana na kuzungumza katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala mbalimbali ya kushirikiana katika ili kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi, kupanua miundombinu na kuharakisha mpango wa taifa wa mabadiliko ya nishati chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (DIRA 2050)..jpg)
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza jambo wakati akiongoza kikao na ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) Kanda ya Afrika Mashariki, ukiongozwa na Mkurugenzi wake, Bi. Mary Porter Peschka, baada ya kukutana na kuzungumza katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala mbalimbali ya kushirikiana katika ili kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi, kupanua miundombinu na kuharakisha mpango wa taifa wa mabadiliko ya nishati chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (DIRA 2050).
Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Mary Porter Peschka, akizungumza jambo wakati wa alipoongoza ujumbe wa IFC kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani), katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala mbalimbali ya kushirikiana katika ili kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi, kupanua miundombinu na kuharakisha mpango wa taifa wa mabadiliko ya nishati chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (DIRA 2050).
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (kulia), akiteta jambo na kiongozi wa ujumbe kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Mary Porter Peschka, mara baada ya kikao chao kilichofanyikakatika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo walijadili masuala mbalimbali ya kushirikiana katika ili kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi, kupanua miundombinu na kuharakisha mpango wa taifa wa mabadiliko ya nishati chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (DIRA 2050).
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiagana na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Mary Porter Peschka, baada ya kukutana na kuzungumza katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, kuhusu masuala mbalimbali ya kushirikiana katika ili kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi, kupanua miundombinu na kuharakisha mpango wa taifa wa mabadiliko ya nishati chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (DIRA 2050).

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Mary Porter Peschka, na maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati, Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), pamoja na wawakilishi wa IFC, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukutana na kufanya mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, kuhusu masuala mbalimbali ya kushirikiana katika ili kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi, kupanua miundombinu na kuharakisha mpango wa taifa wa mabadiliko ya nishati chini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 (DIRA 2050).
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)