Na. OWM- KAM
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Rahma Kisuo amewataka wataalamu na wadau wa Ustawi wa Jamii kufanya kazi kwa weledi, uadilifu katika utendaji kazi hususani kwa watoto na wananchi wanyonge.
Ameyasema hayo Machi 24, 2026 Jijini Dodoma wakati alipofungua Kongamano na Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Ustawi wa Jamii Tanzania (TASWO) huku akiwasisitiza wataalam hao kutumia teknolojia (mifumo ya Kielektroniki) katika utendaji kazi ili kurahisisha ukusanyaji wa taarifa mbalimbali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama wa wataalamu wa Ustawi wa Jamii (TASWO) Dkt. Mariana Makuu akizungumza kwenye kikao hicho alisema kongamano limelenga kuwakutanisha wanataaluma wa huduma za ustawi wa jamii, watunga sera ,wanafunzi na wakufunzi kutoka vyuo vinavyotoa taaluma za ustawi wa jamii ili kujadili kwa pamoja maswala ya kitaalamu kwa lengo kuu la kuboresha elimu ,sera na huduma za utawi wa nchi.