DKT. MWIGULU: TUENDELEE KUMUOMBEA MHE. LUKUVI

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akimfariji, Germina Lukuvi (wa tatu kushoto), mjane wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, William Lukuvi alipokwenda nyumbani kwa marehemu Area D jijini Dodoma kuhani, Machi 26, 2026. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza wakati alipokwenda nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, marehemu William Lukuvi, Area D jijini Dodoma, Machi 26, 2026. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, William Lukuvi, nyumbani kwa marehemu Area D jijini Dodoma, Machi 26, 2026. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akiwafariji watoto wa aliyekua Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, na Wenye Ulemavu, William Lukuvi, Mossy Lukuvi (wa pili kulia na Brown Lukuvi (kulia) nyumbani kwa marehemu Area D jijini Dodoma alipokwenda kuhani, Machi 26, 2026. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Toba Nguvila. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, Naibu Spika Daniel Sillo (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, wakati alikokwenda kuhani msiba nyumbani kwa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, marehemu William Lukuvi, Area D jijini Dodoma, Machi 26, 2026. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewaomba Watanzania waendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, marehemu William Lukuvi aliyefariki jana Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma.

Akiongea kwa niaba ya Serikali nyumbani kwa marehemu Area D, jijini Dodoma leo, Alhamisi, Machi 26, 2026, Waziri Mkuu amesema: β€œKwa niaba ya Serikali natoa pole kwa familia, ndugu, jamaa. Jambo hili zito, gumu kulielewa, gumu kulipokea.”

…Lakini ndio limeshatufika na sote hatukutarajia maana Mheshimiwa Waziri alikuwa kazini. Tuendelee kumuombea kwa Mwenyezi Mungu na kuifariji familia. Mwenyezi Mungu awaimarishe kwa sababu yeyΓ© ndio mfariji mkuu,” amesisitiza.

Vilevile, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametumia fursa hiyo kuihakikishia familia kwamba Serikali itaendelea kuwa pamoja nayo katika kipindi hiki chote cha majonzi.

Viongozi wengine waliokuwepo msibani hapo ni pamoja na Naibu Spika, Daniel Siro, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Masauni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumisi wa Umma na Utawala Bora), Ridhiwani Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Toba Nguvila.