Wakati mashabiki wa soka nchini Tanzania wakiendelea kutafuta majibu ya namna gani timu ya Taifa “Taifa Stars” imepoteza mchezo mbele ya Liechtenstein, Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe, ameibuka na uchambuzi mchungu akidai kuwa kipigo hicho kimesababishwa na tatizo la kisaikolojia zaidi kuliko ufundi.
Licha ya Tanzania kuwa na kikosi chenye “Quality” kubwa na mastaa wanaocheza soka la kulipwa kimataifa, kichapo cha 1-0 dhidi ya timu inayoshika nafasi za chini kwenye viwango vya FIFA kimeelezwa kama “Aibu ya Taifa” inayohitaji somo kubwa.
Ugonjwa wa ‘kuwachukulia poa’
Katika uchambuzi wake, Kamwe amebainisha kuwa wachezaji wa Stars waliingia uwanjani wakiwa na dhana ya ushindi wa mezani kwa kuangalia rekodi mbovu za wapinzani wao badala ya kupambana ndani ya dakika 90.
“Kosa la kwanza lilianzia ‘KICHWANI’ kwa watu wetu kambini… Kichwani kwa wachezaji wetu ikaishi ile kauli ya, ‘Tutawaweka tu hawa’. Kwangu, hii MENTALITY ndio ilikuwa tatizo kubwa sana,” alisema Kamwe.
Takwimu za udhalilishaji: Mashuti 11 Nje ya Lengo
Hoja ya Kamwe inaungwa mkono na takwimu za mchezo huo ambazo zinaonyesha Tanzania ilitawala mpira kwa asilimia 58 dhidi ya 42, lakini ikashindwa kuwa na umakini kwenye eneo la mwisho (final third).
Ali Kamwe amekwenda mbali zaidi na kulinganisha takwimu za mchezo ambazo zinaonyesha wazi kuwa Stars ilikosa umakini kwenye eneo la mwisho. Licha ya kumiliki mpira kwa asilimia 58, ufanisi wa kupiga mashuti ulikuwa wa hovyo.
- Tanzania: Ilimiliki mpira kwa 58%, ikapiga mashuti 14, lakini ni 3 pekee yaliyolenga lango. Mashuti 11 yalipaa nje!
- Liechtenstein: Walimiliki mpira kwa 42%, wakapiga mashuti 4 tu, lakini 3 yalilenga lango na moja likazaa goli.
Hii inamaanisha wapinzani walikuwa na nidhamu ya hali ya juu huku Stars ikicheza kwa “presha” na kukosa utulivu.
Kauli za Gamondi na Novatus Dismas
Baada ya mchezo huo, Kocha Mkuu Miguel Gamondi ameomba radhi Watanzania na kukubali kubeba lawama zote za kiufundi. Kwa upande wake, kiungo fundi Novatus Dismas amekiri kuwa kwa hadhi ya timu ya Tanzania kwa sasa, kufungwa na Liechtenstein ni “AIBU”.
Pamoja na machungu hayo, Ali Kamwe amesisitiza kuwa huu ni wakati wa kujifunza. Amesema kuwa endapo vijana wetu watabadili fikra na kuacha kuangalia rekodi za wapinzani kwenye karatasi, Tanzania bado ina kikosi bora cha kutuhakikishia heshima kwenye AFCON 2027.
Utani pembeni .. Tuzungumze mpira sasa. Ukweli mchungu ni kwamba Tumefungwa na Timu mbovu kwenye ramani ya mpira wa miguu duniani kwa sasa
With all the Quality ambayo tuko nayo kwenye kikosi chetu, walioanza na waliokaa benchi.. Kufungwa na wale Lienchesta sijui, Imeumiza wengi sana
Nini kimesababisha kichapo hiki? Jibu la kwanza liko hapa. Sikiliza mahojiano ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi baada ya mechi
Msikilize pia Kiungo wa mpira, Novatus Dismas baada ya mechi.. Utagundua kuwa Kosa la kwanza lilianzia KICHWANI kwa watu wetu kambini
Gamondi anaomba msamaha Watanzania na amekubali kubeba lawama. Nova amekiri kwa wachezaji kwao kipigo hiki ni AIBU.
Hii AIBU inakuja kwenye vichwa vyao kwa sababu wanajua tumefungwa na Kibonde kwa kuangalia rekodi na Rank za FIFA… Lakini kwa Takwimu za mechi, Wote tulikuwa na SHOTS ON TARGET 3 kila mmoja.
Tofauti ni kwamba, takwimu hizo Sisi Tanzania tulizipata katika majaribio ya MASHUTI 14 na Wapinzani ni Majaribio ya MASHUTI 4 tu.
Yani sisi Tulipiga MASHUTI 11 OFF TARGET na Wazungu walikuwa na OFF TARGET MOJA TU. Hapa ndio Shida ilipo
Ni kama hatukuwa na umakini kabisa uwanjani. Focus ikawa ndogo kwenye maamuzi yetu. Kichwani kwa wachezaji wetu ikaishi ile kauli ya, “Tutawaweka tu hawa”
Kwangu, hii MENTALITY ndio ilikuwa tatizo kubwa sana nje ya Kila kitu. TULIWACHUKULIA POA SANA HAWA WAZUNGU.
Tuliwachukulia poa kwa Rekodi zao Lakini uwanjani Tulifanana nao. Hata umiliki wa mpira, sisi Tulikuwa na 58% wao 42% tu.
Naamini.. Baaada ya kuwasha simu zao muda huu na kusoma comments za Watanzania vijana wetu wakiambiwa rudini tena uwanjani, Hawa wazungu wanakufa hata 5.
Tukubali AIBU lakini Tulibebe hili kama Funzo.
BADO TUNA TIMU NZURI YA KUTUHESHIMISHA AFCON 2027, IN SHAA ALLAH👊🏼🤲🏽