Moshi ukiongezeka kufuatia mlipuko wa bomu katika kitongoji cha Dahieh cha Beirut, Lebanon.
Habari za Umoja wa Mataifa
Ni siku ya 26 ya vita katika Mashariki ya Kati. Mashambulizi yanayoendelea nchini Israel na Iran yamejumuisha kushadidisha mashambulizi ya Israel dhidi ya maeneo yanayolengwa na Hezbollah nchini Lebanon, huku takriban wanajeshi 2,000 wa Marekani wakiripotiwa kukaribia kukusanyika katika eneo hilo. Wakati huo huo, Iran imeliambia shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya baharini kwamba Mlango wa Bahari wa Hormuz bado uko wazi kwa meli “zisizo adui” zisizohusishwa na Marekani na Israel. Huko Geneva, mjadala wa dharura wa nadra juu ya mgogoro pia unaendelea katika Baraza la Haki za Kibinadamu. Endelea kuwa nasi kwa masasisho ya moja kwa moja kutoka kwenye mfumo wa Umoja wa Mataifa. Watumiaji wa programu ya UN News wanaweza kufuatilia habari hapa.