Mashindano ya FIFA Series 2026 Kuanza Leo Rwanda, Stars Kukiwasha

Global Publishers
March 26, 2026
0 Comments

Mashindano ya kimataifa ya soka ya FIFA Series 2026 yanaanza rasmi leo Machi 26, 2026 jijini Kigali, huku Rais wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA), Fabrice Shema, akitangaza zawadi mbalimbali zitakazowania kuanzia kombe la ubingwa hadi tuzo ya mchezaji bora wa mashindano.

FIFA Series ni mpango mpya wa kimataifa ulioanzishwa na FIFA ili kutoa nafasi zaidi kwa timu za taifa kucheza mechi za kimataifa hasa zile ambazo hupata nafasi chache ya kukutana na timu kutoka mabara mengine.

Kuanzia leo, viwanja vya Amahoro na Kigali Pelรฉ vinakuwa kitovu cha soka duniani, huku mataifa nane yakishuka dimbani yakisaka ushindi na kujijengea heshima kimataifa.

Mashindano haya yanakusanya timu kutoka mabara tofauti, yakitoa nafasi kwa timu kujipima uwezo na kuongeza uzoefu wa kimataifa.

Timu shiriki zimepangwa katika makundi mawili

KUNDI A (Uwanja wa Amahoro)ย 
๐Ÿ‡ท๐Ÿ‡ผ Rwanda (Wenyeji)
๐Ÿ‡ฐ๐Ÿ‡ช Kenya
๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ช Estonia
๐Ÿ‡ฌ๐Ÿ‡ฉ Grenada

KUNDI B (Uwanja wa Kigali Pelรฉ)ย 
๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ Tanzania (Taifa Stars)
๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ฎ Liechtenstein
๐Ÿ‡ฆ๐Ÿ‡ผ Aruba
๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ด Macau

Mechi za leo (Machi 26):
๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ Tanzania ๐Ÿ†š ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ฎ Liechtenstein (Uwanja wa Kigali Pelรฉ)

๐Ÿ‡ฆ๐Ÿ‡ผ Aruba ๐Ÿ†š ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ด Macau (Uwanja wa Kigali Pelรฉ)