TCDC NA TAKUKURU  ZASAINI MAKUBALIANO KUPAMBANA NA RUSHWA KWENYE VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI

 

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege,(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila,(kushoto) wakionyesha Mkataba baada ya kusaini   hati ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) hafla iliyofanyika  jijini Dodoma.

…..

TUME  ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa lengo la kuweka utaratibu maalum utakaorahisisha na kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa katika vyama vya ushirika nchini.

Taasisi hizo zimesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU)  jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya juhudi za pamoja za kudhibiti vitendo vya rushwa katika sekta ya ushirika. 

Akizungumza katika hafla hiyo Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege,amesema kuwa makubaliano hayo yanalenga kupunguza na  kuondoa madhara yanayosababishwa na vitendo vya rushwa pamoja na ubadhirifu wa fedha na mali ndani ya vyama vya ushirika.

 “Ushirikiano huo utajikita katika maeneo mawili makuu ambayo ni elimu na mafunzo pamoja na utafiti na uchambuzi wa mifumo. Kupitia elimu, wataandaa programu za pamoja za kuwajengea wadau wa ushirika uelewa kuhusu madhara ya rushwa na kuwahamasisha kushiriki katika mapambano dhidi yake.”amesema Dkt. Ndiege

Kwa upande wa utafiti, taasisi hizo zitafanya uchambuzi wa kina wa mifumo ya utendaji ili kubaini na kuziba mianya ya rushwa mapema.

Aidha Dk. Ndiege amesema kuwa  wataunda kamati ya ufundi yenye wajumbe watatu kutoka kila upande itakayokutana kila robo mwaka. Pia kutakuwa na kamati ya usimamizi itakayoongozwa na watendaji wakuu wa taasisi hizo, itakayokutana mara moja kwa mwaka kufuatilia maendeleo ya utekelezaji.

Hata hivyo ameongeza kuwa rushwa na ubadhirifu wa fedha na mali ndani ya vyama vya ushirika vina madhara makubwa kwa maendeleo ya sekta hiyo.

“Rushwa ni adui wa maendeleo ya vyama vya ushirika na inarudisha nyuma juhudi za wanachama katika kujiletea maendeleo,” amesisitiza Dk. Ndiege.

Amesisitiza kuwa taasisi hizo zimeamua kushirikiana kwa dhati ili kuhakikisha ushirika unasonga mbele na kuchangia katika kukuza uchumi wa wananchi.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila,amesema  Serikali imejipanga kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kupitia mipango na mikakati mbalimbali, ikiwemo kuzuia na kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.

Amesema Tume ya Maendeleo ya Ushirika ni mdau muhimu ambaye kwa muda mrefu amekuwa akishirikiana na TAKUKURU katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali, ikiwemo utafiti, uchambuzi wa mifumo, utoaji wa elimu na kusaidia katika hatua za uchunguzi.

“Tumekuwa tukishirikiana katika kufanya utafiti na uchambuzi wa mifumo, kutoa elimu kwa wadau wa ushirika na pia kupata ushirikiano katika ngazi mbalimbali za uchunguzi,” amesema Chalamila.

Pia ameongeza kuwa kupitia ushirikiano huo, taasisi hizo zitaendelea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kuzuia rushwa ndani ya vyama vya ushirika.

Aidha, wataandaa programu za pamoja za elimu, kufanya tafiti za mifumo ya utendaji wa vyama vya ushirika, pamoja na kuandaa vikao kazi vya kujadili matokeo ya tafiti hizo na kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia vitendo vya rushwa.

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege,akizungumza wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),iliyofanyika jijini Dodoma.

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege,akizungumza wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila,akizungumza wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) na  Tume ya Maendeleo ya Ushirika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila,akizungumza wakati wa hafla ya kusaini hati ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) na  Tume ya Maendeleo ya Ushirika hafla iliyofanyika jijini Dodoma.

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege,(kulia) akisaini  hati ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila,(kushoto)  hafla iliyofanyika  jijini Dodoma.

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege,(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila,(kushoto) wakionyesha Mkataba baada ya kusaini   hati ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) hafla iliyofanyika  jijini Dodoma.

Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege, na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini   hati ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) hafla iliyofanyika  jijini Dodoma.