Video: Meneja wa Simba Afunguka Kuhusu Mchezaji Sowah

Bakari Mahundu
March 26, 2026
0 Comments

Meneja wa timu ya Simba SC, Patrick Rweyemamu, amefafanua kuwa suala linalomhusu mchezaji Sowah ndani ya klabu hiyo bado linaendelea kushughulikiwa na Kamati ya Nidhamu ya klabu.

Rweyemamu amesema kuwa kamati hiyo inaendelea kupitia kwa kina tukio hilo kabla ya kufikia maamuzi ya mwisho, akisisitiza kuwa uongozi wa Simba unafuata taratibu zote za kikanuni ili kuhakikisha haki inatendeka kwa pande zote husika.

Ameongeza kuwa mara baada ya mchakato huo kukamilika, Kamati ya Nidhamu itatoa ripoti rasmi pamoja na uamuzi wa mwisho ambao utawekwa wazi kwa umma.

Hata hivyo, hakutoa maelezo ya kina kuhusu chanzo cha suala hilo, akibainisha kuwa ni vyema kusubiri maamuzi ya kamati husika ili kuepusha upotoshaji wa taarifa.