Live: Viongozi, Wananchi Wajitokeza Kuaga Mwili wa Lukuvi Viwanja vya Bunge Dodoma

Global Publishers
March 27, 2026
0 Comments

Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba

Shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Isimani, William Lukuvi, inafanyika leo Machi 27, 2026 katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Shughuli hiyo inatarajiwa kuhusisha viongozi mbalimbali wa serikali, wabunge pamoja na wananchi waliofika kutoa heshima za mwisho kwa marehemu huyo aliyewahi kulitumikia taifa katika nyadhifa mbalimbali za uongozi.

Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kuwaongoza viongozi hao pamoja na wananchi katika shughuli hiyo ya heshima ya kumuaga marehemu Lukuvi.

Baada ya shughuli ya kuaga kumalizika Dodoma, mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam, ambako pia utaagwa tena katika Viwanja vya Karimjee kesho, Machi 28, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi, marehemu William Lukuvi alifariki dunia Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mazishi ya kiongozi huyo yanatarajiwa kufanyika Jumanne, Machi 31, 2026 katika Kijiji cha Idodi, wilayani Iringa Vijijini, ambapo familia, viongozi wa serikali na wananchi mbalimbali wanatarajiwa kushiriki kumlaza katika nyumba yake ya milele.