Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.
******
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amewahimiza wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kupata matibabu bure.
Huduma hiyo inatolewa katika Kituo cha Biashara cha Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo.
Akizungumza wakati wa ziara yake, Prof. Mkumbo amesema kambi hiyo inalenga kusaidia wananchi kupata huduma za afya bila gharama.
Amesema pia kuna vipimo vya kisasa vinavyotolewa na madaktari kutoka China.
Kambi hiyo imeanza Machi 28 na inatarajiwa kumalizika Machi 29, 2026.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa EACLC, Cathy Wang, amesema wameamua kuandaa kambi hiyo ili kurudisha kwa jamii.
Mkurugenzi wa EACLC, Cathy Wang
Amesema biashara lazima iendane na kuwahudumia wananchi wanaowazunguka.
Baadhi ya wananchi waliopata huduma, akiwemo Shabani Said, wamesema huduma ni nzuri na imewasaidia.
Naye Rose Muhaya ameomba muda wa kambi uongezwe kutokana na idadi kubwa ya watu wanaojitokeza.
Wamesema siku mbili hazitoshi kuhudumia wananchi wote wanaohitaji matibabu.
Wakazi wa Dar es Salaam walivyojitokeza kwa wingi kupata matibabu bure leo katika Kituo cha Biashara cha Afrika Mashariki (EACLC) kilichopo Ubungo.


