MAHUBIRI: Kanuni tano za Kimungu kushinda tamaa za mwili
Wapendwa katika Kristo, Bwana Yesu asifiwe. Leo tunaangalia somo muhimu katika maisha ya Mkristo: jinsi ya kushinda tamaa ya mwili. Ukweli ni kwamba tamaa ya mwili ina nguvu, hasa kwa mtu ambaye hajaokoka kikamilifu au hajamruhusu Mungu kutawala maisha yake yote. Tamaa hizi zinaweza kumfanya mtu aishi maisha ya kushindwa, hatia na kujitenga na Mungu,…