Mabula alizwa na ishu ya waamuzi Azerbaijan

Kiungo wa Mtanzania anayeitumikia Shamakhi ya Ligi Kuu Azerbaijan, Alphonce Mabula amesema changamoto ya waamuzi katika mechi za mashindano haipo Bara pekee, bali ipo hadi kwenye anayocheza.

Kumekuwa na malalamiko kwa waamuzi wa mechi mbalimbali hapa nchini, na Mabula amedai kwamba suala hilo siyo la Tanzania pekee kwani hata Azerbaijan hutokea.

Akitoa mfano, amesema kuna tukio lilitokea Machi 18 wakati Shamakhi ilipocheza dhidi ya Araz Naxcıvan ambapo wao walikuwa nyumbani alifunga bao, lakini mwamuzi akaamua kukataa na pia kuwanyima penalti ya wazi. Mchezo huo ulimalizika Shamakhi wakipotez kwa bao 1-0. Akielezea tukio hilo, Mabula amesema: “Nilitoa pasi nzuri kwa mshambuliaji, akaangushwa wazi kabisa ndani ya boksi, lakini mwamuzi akaona ni kama chalenji ya kawaida.”

Kitu kilichowauma zaidi kwa mujibu wa Mabula ni kwamba, mwamuzi hakutaka kutumia teknolojia ya VAR Mabula aliongeza kuwa, “kama (mwamuzi) angeenda kuangalia VAR naamini kabisa angebadili uamuzi. Tulinyimwa haki yetu. Refa katuua sana. Tulistahili penalti, lakini hakutaka hata kwenda kuangalia VAR.”

Huu ni msimu wa pili kwa Mabula kuitumikia Shamakhi ambapo alijiunga na chama hilo wakati dirisha dogo la msimu uliopita akitokea Spartak Subostica ya Serbia.