Meneja Bidhaa wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Bryton Kimemeta (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanawake wajasiriamali, wanachama wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, katika semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa uwezeshaji wa benki hiyo ikihusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo hayo ni sehemu ya mikakati ya Benki ya Absa ya kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo inayosema ‘Stori yako ni ya thamani’.
Meneja Msaidizi wa Uhakiki wa Biashara wa Benki ya Absa Tanzania. Bi. Miriam Ngajilo (kushoto), akizungumza na baadhi ya wanawake wajasiriamali, wanachama wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, katika semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa uwezeshaji wa benki hiyo ikihusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo ya kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la Benki ya Absa la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo inayosema ‘Stori yako ni ya thamani’.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, Bw. Hafizur Milon (kushoto), akizungumza kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya taasisi hiyo na Benki ya Absa Tanzania, wakati wa semina ya wanawake wajasiriamali wanachama wa taasisi hiyo kuhusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya Benki ya Absa katika kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la ‘Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine’, kupitia chapa ya benki hiyo inayosema ‘Stori yako ni ya thamani’.