OFISI YA MAKAMU WA RAIS NA JIJI LA DAR ES SALAAM ZAKUBALIANA KUANDAA MAKUBALIANO KUANZIA KITUO CHA KUMBUKUMBU ZA MUUNGANO

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Bi. Cesilia Nkwamu akiwasilisha maelezo kuhusu andiko la ukumbi wa Karimjee kuwa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi) wakati wa kikao baina ya wataalamu kutoka Ofisi hiyo, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kilichofanyika Machi 31, 2026 Jijini Dar es Salaam.

**************


Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam zimekubaliana kuandaa Hati ya Makubaliano (MoU) kwa ajili ya kuufanya Ukumbi wa Karimjee kuwa Sehemu ya Kituo cha Kutunza Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi).

Akizungumza katika kikao baina ya wataalamu wa Ofisi hizo Machi 31, 2026 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Juma Mohammed Salum amesema makubaliano hayo ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Salum amesema Ofisi ya Makamu wa Rais ilipewa maelekezo mahsusi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuanzisha Vituo Vya Kutunza Kumbukumbu na nyaraka Muungano (Makavazi) upande wa Tanzania Bara na Zanzibar ili kusaidia wananchi kuelewa chimbuko na misingi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

“Makubaliano hayo yataweka msingi muhimu katika kutunza historia ya taifa letu kwani ukumbi wa karimjee ni moja ya eneo muhimu na sote kama tunavyokumbuka ndipo ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilizaliwa mwaka 1964” amesema Dkt. Salum.

Aidha Dkt. Salum amesema makubaliano hayo pia yatawezesha utunzaji na uhifadhi wa taarifa muhimu za Muungano ambazo ni muhimu kwa ajili ya mustakabali wa kizazi cha sasa na baadae na kuwa hatua hiyo inawezesha wananchi kufahamu manufaa ya Muungano.

“Zipo baadhi ya nchi duniani ikiwemo Ujerumani soko la historia ni muhimu sana kwa wanafunzi wa taifa hilo, hivyo sisi tumeona ni muhimu kutunza historia ya taifa letu kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo” amesema Dkt. Salum.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bw. Elihuruma Mabelya ameishukuru Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuandaa andiko hilo na kuwa Ofisi yake itatoa ushirikiano unaohitajika ili kufanikisha wazo hilo ambalo ni muhimu kwa mustakabali wa taifa.

“Tunashukuru kwa wazo hili ambalo sisi kama Jiji tutahakikisha linapitia ngazi zote za maamuzi ikiwemo kujadiliwa na kupitishwa katika vikao vya Baraza la Madiwani ili kupata baraka na hatimaye kuanza utekelezaji” amesema Elihuruma.

Aidha Elihuruma alishauri kuundwa kwa kamati ndogo ya wataalamu kwa ajili ya kuratibu mpango kazi utakaondaliwa ambao utaongeza kasi ya utekelezaji wa malekezo yanayotolewa katika ngazi za maamuzi.

Kikao hicho cha siku moja kiliwashirikisha wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.

Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Juma Mohammed Salum akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kilichofanyika Machi 31, 2026 Jijini Dar es Salaam ambacho kilijadili andiko la ukumbi wa Karimjee kuwa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi).

Baadhi ya wajumbe wa kikao kilichojadili kuhusu andiko la ukumbi wa Karimjee kuwa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi) kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakifuatilia majadiliano ya kikao hicho kilichofanyika Machi 31, 2026 Jijini Dar es Salaam ambacho kilijadili andiko la ukumbi wa Karimjee kuwa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano

Wajumbe wa kikao ya wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika kikao kilichojadili andiko la ukumbi wa Karimjee kuwa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi).

Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Dustan Shimbo akizungumza jambo wakati wa kikao baina  ya wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kilichofanyika Machi 31, 2026 Jijini Dar es Salaam ambacho andiko la ukumbi wa Karimjee kuwa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi).

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bw. Elihuruma Mabelya akizungumza jambo wakati wa kikao baina  ya wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kilichofanyika Machi 31, 2026 Jijini Dar es Salaam ambacho kilijadili andiko la ukumbi wa Karimjee kuwa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi).

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Sarah Kibonde akizungumza jambo wakati wa kikao baina  ya wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kilichofanyika Machi 31, 2026 Jijini Dar es Salaam ambacho kilijadili andiko la ukumbi wa Karimjee kuwa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi).

Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Joyce Mnunguli akizungumza jambo wakati wa kikao baina  ya wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kilichofanyika Machi 31, 2026 Jijini Dar es Salaam ambacho kilijadili andiko la ukumbi wa Karimjee kuwa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi)

Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Juma Mohammed Salum (kushoto mbele) akiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bw. Elihuruma Mabelya (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kikao kilichojadili andiko la ukumbi wa Karimjee kuwa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano (Makavazi) kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kilichofanyika Machi 31, 2026 Jijini Dar es Salaam.