DAR ES-SALAAM:
Hospitali ya kumbukumbu ya Dr Ole Lengine, Dr Ole Lengine Memorial Hospital iliyopo Kibamba jijini Dar EsSalaam imezindua gari maalumu la kisasa la kubebea wagonjwa(Ambulance) ili kutatua changamoto zinazowakabili wagonjwa wasiojiweza katika eneo hilo na maeneo ya jirani.
Awali akizungumza na waandishi wa habari, wageni na wananchi waliofika hospitalini hapo kushuhudia uzinduzi huo, Mchungaji Ezekiel Ngao amesema ujio wa gari hilo ni sehemu ya kuimarisha vita dhidi ya maradhi na afya kwa binadamu na kurejesha tumaini jipya kwa wale waliokata tamaa.
“wagonjwa wengi wanapoteza maisha kwa kukosa huduma stahiki ya dharura kabla ya kufika hospitalini na mara nyingi hutokana na kukosa gari maalum la wagonjwa lenye fifaa tiba, madawa na watoa huduma ya dharura ya kiafya” Mchungaji Ngao amesema hayo mara baada ya kuongoza zoezi zima la uzinduzi huku akitoa wito kwa serikali kuisaidia sekta binafsi wanaowekeza katika eneo la afya kwani wanachangia sana uzalishaji wa nguvu kazi ya taifa la sasa la kesho.
Dr Felister Kimolo ni mmoja kati wajumbe toka sekta ya afya waliohudhuria tukio la uzinduzi wa gari hilo ambapo amesema gari hilo litasaidia sio tu wagonjwa wanaofika hospitalini hapo bali pia wale wanaotoka katika vituo vya afaya vya jirani, wajumbani na wale wanaopata ajali katika mikoa ya jirani na kwingineko kulingana na mahitaji ya huduma hiyo kwa wakati huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Dr Ole Memorial Hospital, Betha Emmanuel amesema ujio wa gari hilo ni sehemu ya kuiunga mkono serika katika jitihada zake za kusogeza karibu huduma za kiafya kwa wananchi na kwamba gari hilo litasaidia kutoa huduma ya dharura katika maeneo yanayopatwa na majanga mbalimbali kama moto, mafuriko na ajali.
Naye Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa hospitali hiyo Dr Emmanuel Ole Lengine amesema hospitali hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali kupitia sekta ya afya katika kuboresha huduma za afya ambapo baada ya gari hilo, ni mwanzo wa maandalizi ya uboreshaji wa huduma zingingine za dharura yaani Emergency service. Dr Emmanuel amesema hayo huku akielekeza msisitizo kwa wauguzi hususani wa kitengo cha huduma ya dharura (Emergency) kuwa sehemu ya matumaini kwa wagonjwa wanafika kupata huduma hiyo.
Mchungaji Ezekiel Ngao akikata utepe kuashiria kuzindulia rasmi kwa gari maalum la kisasa la kubebe wagonjwa katika hospitali ya kumbukumbu ya Dr Ole Lengine.
(Kushoto kwake ni CEO wa Hospitali hiyo Dr Emmanuel Ole Lengine, katikati ni Dr Felister Kimolo kutoka manispaa ya Ubungo na kulia ni Mkurugenzi wa Dr Ole Lengine Memorial Hospital, Bertha Emmanuel.
C.E.O wa Dr Ole Lengine Memorial Hospital Dr Emmanuel Ole Lengine katikati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa gari maalum la kisasa la kubebea wagonjwa.


