Dk Mwigulu atoa maagizo mapya utatuzi wa kero za wananchi
Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuhamia kwa ofisi zote za umma katika Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma kunapaswa kurahisisha utoaji wa huduma na kushughulikia kero za wananchi kwa haraka na ufanisi. Amesema badala ya kuandikiana barua zinazoongeza urasimu, watumishi wa umma wanapaswa kukutana ana kwa ana ili kutatua changamoto zinazohusu wananchi…