Utafiti waonya utegemezi wa Dar kwa mapato ya kodi
Dar es Salaam. Wakati takwimu zikionesha asilimia 70 ya mapato ya kodi nchini kukusanywa katika Jiji la Dar es Salaam, utafiti mpya umeonya kuwa utegemezi mkubwa wa mkoa mmoja si endelevu na unaweza kuathiri azma ya Tanzania kufikia uchumi wa dola trilioni moja ifikapo mwaka 2050. Utafiti huo unapendekeza kufanyika kwa mageuzi ya kina yatakayohamasisha…