FYATU MFYATUZI: Tulaani na kudunisha udini wa dini zetu
Fyatuland ina visa, visasi, vitimbi, vitimbwiliko usipime. Japo, tunaonyesha kuyanyamazia na kuwashabikia, kuna mafyatu wanaofyatuka hovyo hovyo wakicheleta na kuchezea hatari wasijue zahama wanayotengeza. Wapo mafyatu uchwara waliojipa, sijui kupewa vibali vya ‘kuvuruga’ amani wakidai na kujifanya wanaitetea. Sijui nani huyu mchizani anayewatuma hawa wahuni, apate nini, na iwe nini? Nijuavyo, dini ni suala la…