Rais Samia aeleza sababu za kumteua Profesa Kabudi

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan, ameweka wazi sababu za kumteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Ikulu (Kazi Maalumu). Kabla ya uteuzi, Profesa Kabudi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Rais amesema uamuzi huo umetokana na mahitaji mapya ya uendeshaji wa Serikali katika mazingira ya siasa…

Read More

Mtunisia Azam anukia Irak | Mwanaspoti

KLABU ya Azam huenda ikaachana na winga Mtunisia Baraket Hmidi, baada ya mchezaji huyo kushindwa kulishawishi benchi la ufundi la timu hiyo chini ya Kocha Mkongomani Florent Ibenge tangu asajiliwe. Nyota huyo aliyejiunga rasmi na Azam, Agosti 16, 2025, akitokea CS Sfaxien ya kwao Tunisia, inadaiwa ataondolewa katika dirisha hili dogo la Januari, ambapo hadi…

Read More

Samia akutana na Taifa Stars Dar

RAIS Samia Saluhu Hassan ameipongeza timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kwa kufika 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), inayoendelea huko Morocco. Stars iliyokuwa inashiriki mashindano hayo kwa mara ya nne ilitolewa na Morocco kwa kuchapwa bao 1-0, ingawa imeweka rekodi ikiwa ni mara ya kwanza inafika hatua hiyo kwani mara tatu…

Read More

Askofu Temu: Kuweni Majasiri kusema ukweli, kupigania haki

Dar es Salaam. Abate wa Abasia ya Ndanda wa Kanisa Katoliki, Christian Temu amesema Wakristo wanapaswa kutambua kuwa woga si jambo la kuchagua, bali wanawajibika kuwa wajasiri, kupenda kusema na kusimamia ukweli na kuzungumzia masuala ya haki bila kuogopa. Abate Temu amesema hayo ni kwa sababu haki na amani ni matunda ya Kimungu yasiyotengenezwa na…

Read More

Sakata Mwandambo kukamatwa Mbeya, kushtakiwa na kuachiwa Dar

Dar es Salaam. Wakati mawakili wa mtengeneza maudhui mtandaoni, Clemence Mwandambo, wakifungua shauri Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mbeya, kuomba amri afikishwe mahakamani, tayari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Temeke na kuachiwa kwa dhamana. Mwandambo, mwalimu wa Shule ya Awali ya St. Clemence, amekuwa maarufu mitandaoni kutokana na maudhui yake yenye kibwagizo: “Nachoka baba yenu Clemence…

Read More