Simba yaachana na straika | Mwanaspoti

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Simba Queens, Magnifique Umutesiwase amerejea nchini kwao Rwanda kujiunga na Indahangarwa inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake huko. Hatua hiyo ya Magnifique inakuja miezi michache baada ya Simba Queens kuamua kuachana naye mwishoni mwa mwaka jana ikidaiwa alishindwa kuendana na kasi pamoja na mahitaji ya kikosi hicho, hususan katika eneo la ushambuliaji. Magnifique…

Read More

Wakenya waingilia dili la Awesu

WAKATI Klabu ya Mbeya City ikiwa katika mazungumzo ya kupata saini ya kiungo mshambuliaji wa Simba, Awesu Ally Awesu, uongozi wa Kenya Police ya Kenya, umeingilia kati dili hilo kwa ajili ya kumpata nyota huyo kwa mkopo wa miezi sita. Kenya Police ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi ya Kenya msimu uliopita, wamefungua mazungumzo hayo…

Read More

Tanroads Kigoma yatangaza donge kwa watakaofanikisha kukamatwa kwa wezi

Kigoma. Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani Kigoma, imetangaza zawadi kwa mwananchi atakayefanikisha kukamatwa kwa wezi wanaoiba vyuma vinavyoonesha alama za barabarani mkoani humo. Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa Januari 10, 2026 na ofisi ya Meneja wa Tanroads Mkoa wa Kigoma Mhandiai Narcis Choma yeyote atakayefanikisha au kutoa ushahidi huo atapewa zawadi mpaka Sh150,000  kulingana…

Read More

UDOM yakanusha madai ya wanafunzi kulipia vyumba hewa

Dodoma. Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), umekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari zikieleza uwepo wa changamoto ya uhaba wa mabweni kwa wanafunzi chuoni hapo. Hayo yanajiri kufuatia malalamiko yaliotolewa na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wiki iliyopita kupitia mitandao ya kijamii wakidai kuwa wanazimika kulala zaidi ya…

Read More

Johola aanika mambo manne yanayombeba Bara

KIPA wa zamani wa Yanga anayekipiga kwa sasa Mashujaa akiwa ndiye kinara wa ‘cleansheet’ katika Ligi Kuu Bara, Erick Johola amesema ubora alionao unatokana na mambo manne ikiwamo kujiamini, kupambana, nidhamu na kuonyesha kila unapopewa nafasi na kuaminiwa na benchi la ufundi. Kipa huyo anaongoza ya makipa waliokomaa mechi nyingi bila kuruhusu bao akiwa na…

Read More

Stanbic yatajwa tena benki bora Tanzania mwaka 2025

Dar es Salaam. Kwa mara nyingine tena Stanbic imetajwa kuwa Benki Bora zaidi Tanzania kwa mwaka 2025 na jarida la The Banker, chapisho la kimataifa la masuala ya benki chini ya Financial Times. Tuzo hii inatambua utendaji mzuri wa kifedha wa benki, ubunifu na mchango wake endelevu katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania na hii…

Read More

Kiungo kiraka ajipa kazi Geita Gold

KIUNGO mpya kiraka wa Geita Gold, Raymond Masota amesema ujio wake ndani ya timu hiyo unaiongezea nguvu katika mapambano ya kupanda daraja kwenda Ligi Kuu Bara, huku akiahidi kuisaidia ili lengo hilo litimie. Masota anayemudu kucheza nafasi ya winga, kiungo mshambuliaji na beki wa kulia, alijiunga na Geita Gold Januari 8, mwaka huu katika usajili…

Read More

Straika Singida Black Stars atimkia Ureno

MSHAMBULIAJI nyota wa Singida Black Stars, Mzambia Andrew Phiri, ameenda Ureno katika majaribio katika timu ya Clube Desportivo Nacional, baada ya uongozi wa kikosi hicho kumridhia kwa lengo la kwenda kujaribu bahati yake barani Ulaya. Phiri aliyejiunga na kikosi hicho Agosti 26, 2025, akitokea Maestro United ya kwao Zambia, mkataba wake unafikia tamati rasmi Juni…

Read More

Alliance Girls yajipanga kubakiza pointi nyumbani

KOCHA wa Alliance Girls, Sultan Juma amesema kikosi hicho kimeweka mikakati ya kuhakikisha kinabakiza pointi tatu katika michezo yote ya nyumbani watakaocheza Uwanja wa Nyamagana, Mwanza ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kufanya vizuri katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Wanawake. Msimu uliopita Alliance Girls ilimaliza ligi katika nafasi ya nane, ikiwa na pointi…

Read More