TRA yaanza kufanyia kazi maagizo ya Rais Samia

Arusha. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitaka mamlaka hiyo kuongeza wigo wa utoaji huduma wilayani Karatu, Mkoa wa Arusha. Rais Samia alitoa maagizo hayo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2025 akisema ndani ya siku 100 za utawala wake ataongeza wigo wa huduma za kodi. Jana…

Read More

Ukosefu wa vyoo kuwang’oa wakurugenzi, ma-DAS

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, amewabana mawaziri wanne na manaibu wao kujibu hoja zilizotolewa na Mbunge wa Mkinga, Twaha Mwakioja, huku akiwaagiza wakuu wa mikoa, wakurugenzi kuhakikisha shule, vituo vya afya vinakuwa na matundu ya vyoo kabla ya tathmini ya utekelezaji wa bajeti 2026/27. Hatua hiyo ilikuja baada ya mbunge huyo kuibua masuala…

Read More

Mholanzi aonyesha pa kuanzia Simba

UNAMKUMBUKA kocha wa zamani wa Yanga, Hans Pluijm? Sasa Mholanzi huyo anayeishi Ghana amevunja ukimya kwa kuichambua Simba kwa namna alivyoifuatilia katika mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika na kutoa sababu kwa nini haijaingia robo fainali ya michuano hiyo licha ya kuwa na wachezaji bora. …

Read More

Askofu Kasala ashauri jambo Bima ya Afya kwa Wote

Geita. Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita, Flavian Kasala ameshauri utaratibu wa utoaji wa Bima ya Afya kwa Wote nchini uzingatie haki na upendo, bila kuweka madaraja yanayosababisha utengano baina ya wanajamii. Ameongeza kuwa ugunduzi wa kitabibu unaofanyika duniani, unalenga kuwanufaisha watu wote bila kujali madaraja ya vipato vyao ambapo amesema anatiwa shaka na tafsiri…

Read More

Kamati ya Bunge yatoa maagizo udhibiti wa bandari bubu nchini

Dar es Salaam. Kushamiri kwa bandari bubu nchini, kumeiamsha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kutoa maagizo kwa Serikali kuweka mkakati wa kudhibiti bandari hizo, kwani ndio lango la uingizwaji wa dawa za kulevya. Mbali na dawa kulevya, kamati hiyo imesema bandari bubu ni uchochoro unaotumika kupitisha bidhaa zisizohitajika nchini. Kauli hiyo inakuja wakati…

Read More

RAIS DKT. SAMIA AREJEA NCHINI AKITOKEA ADDIS ABABA AMBAPO ALISHIRIKI KWENYE MKUTANO WA KAWAIDA WA 39 WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI YA AU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili Kiwanja che Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume, Zanzibar na kupokelewa na Viongozi mbalimbali akitokea nchini Ethiopia baada ya kukamilisha ziara ya kikazi ya siku nne, ambapo pamoja na mambo mengine alishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja…

Read More