Machinga, bodaboda wapaza sauti kero za mikopo asilimia 10, Mwigulu akiri kuna shida

Dar es Salaam. Wakati wamachinga, mama lishe na waendesha bodaboda nchini wakilalamikia masharti magumu ya upatikanaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali, Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, ameweka bayana kuwa fedha hizo awali zilikuwa zikinufaisha makundi ambayo hayakukusudiwa. Amesema vikundi vingine vilinufaika na mikopo hiyo licha ya kutokidhi vigezo, huku baadhi yao vikibainika…

Read More

CCM yaibuka kidedea kortini, barua ya Chongolo ikitajwa

Sumbawanga. Ni mgogoro wa umiliki wa ardhi ulioibuka miaka 40 iliyopita lakini sasa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga, imewapa ushindi Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kuendelea kumiliki eneo hilo. Hii ni baada ya Jaji, Abubakar Mrisha kutoa uamuzi wake Januari 7,2026 katika shauri hilo ambalo barua ya aliyewahi kuwa Katibu…

Read More

Shauri la ACT-Wazalendo kupinga ubunge Lindi Mjini lafutwa

Arusha. Mahakama Kuu Masjala Ndogo Mtwara, imefuta shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge Lindi Mjini. Shauri hilo la uchaguzi namba 30403/2025 lilifunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge jimboni humo kupitia Chama cha ACT- Wazalendo, Mchinjita Isihaka. Walalamikiwa katika shauri hilo walikuwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Lindi Mjini (mlalamikiwa wa kwanza), Mohamed Utaly na…

Read More

Wadau walalamikia kanuni za kudhibiti uchovu wa madereva

Dar es Salaam. Wadau wa usafirishaji wametoa maoni kwa baadhi ya vipengele vya Kanuni za Kudhibiti Uchovu wa Madereva za mwaka 2026, wakisema vinawakandamiza madereva na wamiliki kutokana na changamoto kadhaa za kisheria na kiutendaji zinazopaswa kufanyiwa kazi kabla ya kanuni hizo kupitishwa. Kifungu cha 45(2)(1) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini, Sura…

Read More

Ludewa kugeukia kilimo cha ufuta

Njombe. Zaidi ya wananchi 450 kutoka vijiji vya Tarafa za Masasi na Mwambao wilayani Ludewa, wameanza kunufaika na mgao wa kilo 225 za mbegu bora za ufuta zinazotolewa bure na Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, mkoani Njombe. Hii ni sehemu ya mkakati wa kuwawezesha wananchi wa ukanda huo kiuchumi na kuongeza uzalishaji wa mazao ya…

Read More

Pwani yajipanga ushindani kimataifa uwekezaji wa viwanda

Kibaha. Mkoa wa Pwani umeanza kuchukua hatua mahsusi za kujipanga kuingia katika ushindani wa kimataifa wa maendeleo ya kiuchumi kwa kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji wa viwanda. Akizungumza katika kikao kazi kilichofanyika leo Alhamisi Januari 8, 2026 mjini Kibaha, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amesema mkoa huo umeanza kujiandaa kushindana kimataifa katika kuvutia…

Read More