Dili la kipa mpya Simba ugumu uko hapa

SIMBA inaendelea kuhusishwa kuwapigia hesabu makipa wawili wazawa, Yona Amos wa Pamba Jiji na Patrick Munthary wa Mashujaa ili kuongeza nguvu ikiwa na pengo la Moussa Camara na Yakoub Suleiman ambao ni majeruhi wanaodaiwa watakuwa nje kwa muda mrefu. Hata hivyo, makipa hao nao wameibuka na yao, ikielezwa ni ngumu kwa Munthary sasa kutua Msimbazi…

Read More

Upelelezi kesi ya kusafirisha vinyonga mbioni kukamilika

Dar es Salaam. Upelelezi wa kesi ya kusafirisha vinyonga 164, mijusi 20 na nyoka sita, inayomkabili mshtakiwa Eric Ayo na wenzake wawili, upo hatua za mwisho kukamilika. Wakili wa Serikali, Winiwa Kasala ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo wakati kesi hiyi ilipoitwa kwa kutajwa. Ayo na wenzake wawili wanakabaliwa na kesi ya Uhujumu Uchumi…

Read More

Othman ataka Taifa lijengwe juu ya haki, Katiba 2026

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taifa wa ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman, ametumia salamu za Mwaka Mpya 2026 kuwataka Watanzania kuutumia kama fursa ya kuliponya Taifa, kurejesha misingi ya Katiba na kujenga umoja wa kitaifa unaotokana na haki, uwajibikaji na ridhaa ya wananchi. Katika salamu alizozitoa Januari mosi, 2026, amesema licha ya majaribu, mitihani na maafa…

Read More

Miili sita ajali ya Moro kutambuliwa kwa DNA

Morogoro.  Siku tatu tangu kutokea ajali iliyoua watu 10 mkoani Morogoro, ni miili minne pekee iliyotambuliwa, hali inayolazimu uchunguzi wa vinasaba (DNA) kutumika katika utambuzi kutokana na kuungua kwa kiasi kikubwa. Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Dk Joseph Kway, amesema tayari timu ya wataalamu kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali…

Read More