Tanzania inavyosimama kama moyo wa biashara za kikanda

Tanzania kwa sasa inajikuta katika kipindi cha kipekee cha kihistoria, ikiwa ni nchi pekee mwanachama inayounganisha Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa ufanisi mkubwa. Nafasi hii ya kijiografia si tu zawadi ya asili, bali ni karata muhimu ya kiuchumi ambayo ikitumiwa vyema inaweza kuifanya nchi kuwa…

Read More

‘Pasiwedi’ yazua tuhuma za Thadei Kweka

Moshi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imetoa amri ikimwamuru Thadei Kweka, anayedaiwa kuwa raia wa Marekani, kutoa nywila (password) katika simu yake ili Polisi waendelee na uchunguzi wa tuhuma za jinai zinazomkabili. Amri hiyo imetolewa Desemba 31, 2025, na Hakimu Mkuu Mkazi, Herieth Mhenga, alipotoa uamuzi wa maombi ya jinai namba 000030237 ya 2025, yaliyowasilishwa…

Read More

Maoni mseto hotuba ya Samia mwaka mpya

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoa hotuba ya kufunga mwaka 2025 iliyolenga kujenga umoja wa kitaifa, wachambuzi wa siasa wametoa maoni tofauti, baadhi yao wakieleza kwamba azma yake ya kujenga umoja wa kitaifa imechelewa. Jana, Jumatano Desemba 31, 2025, katika hotuba yake ya kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka 2026,…

Read More

Tato yataja mbinu mpya kuimarisha sekta ya utalii 2026

Arusha. Chama cha Waendeshaji Watalii Tanzania (Tato) kimezitaka taasisi, wawekezaji na wadau wa sekta ya utalii nchini kuwekeza katika ujenzi na uwasilishaji wa simulizi zenye nguvu kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo nchini. Kimesema kwa kufanya hivyo kutaongeza ushindani wa Tanzania katika soko la kimataifa na kukuza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa taifa. Wito…

Read More

Bei ya mchele Mbeya haishikiki, serikali yaingilia kati

Mbeya. Bei ya mchele katika masoko ya jijini Mbeya imeendelea kupanda, hali inayosababisha malalamiko miongoni mwa wananchi huku wataalamu wa uchumi wakieleza sababu za mabadiliko hayo na kuonesha matumaini kuwa hali inaweza kurejea kawaida ifikapo Mei, mwaka huu. Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa wazalishaji wakuu wa zao la mpunga nchini, hususan katika wilaya za…

Read More

Uganda, mataifa mengine 39 duniani kufanya uchaguzi mwaka 2026

Dar es Salaam. Ni mwaka wa uchaguzi. Hivyo ndivyo unavyoweza kuuelezea mwaka 2026 katika ulingo wa siasa za kijiografia kwa sababu mataifa 40 duniani yanatarajiwa kufanya uchaguzi mwaka huu ili kupata viongozi watakaoziongoza serikali zake. Baadhi ya mataifa hayo yatafanya uchaguzi mkuu wa kuwapata Rais, wabunge na madiwani huku nchi nyingine zikitarajia kufanya uchaguzi wa…

Read More

‘Amani ni mbolea ya mafanikio’

Arusha/Manyara. Watanzania wametakiwa kuendelea kumuomba Mungu ili amani iendelee kudumishwa nchini, wakikumbushwa kuwa amani ni msingi muhimu unaochochea mafanikio na ustawi wa jamii. Wito huo umetolewa leo Alhamisi, Januari Mosi, 2026 na Naibu Katibu Mkuu wa Misioni na Uinjilisti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Mchungaji Julius Tarakwa alipokuwa…

Read More