NIKWAMBIE MAMA: Viongozi zingatieni sheria za Tanzania
Kitu kikubwa ambacho wazee wetu hawakukijua, kwenye michezo yetu ya utotoni tuliigiza tabia za baba zetu. Mtoto wa mfanyakazi aliigiza kama mfanyakazi, kadhalika wa mkulima pia aliigiza hivyo. Sipati picha kama mlevi angegundua kuwa mwanaye anamuigiza hadharani kwenye michezo. Bila shaka mtoto huyo angekiona kilichomtoa nyoka miguu, na si ajabu ungelikuwa ndio mwisho wake kucheza….