RIPOTI MAALUMU: Hatari ya kiafya kukosekana vyoo mpakani Tunduma
Dar es Salaam. Ingawa kila lori hutozwa ushuru wa Sh15, 000 kuvuka mpaka wa Tanzania na Zambia kwa ajili ya huduma za jamii, madereva wa malori hayo wanalalamikia kukosekana vyoo vya umma, hali inayowalazimu kuomba huduma hiyo katika nyumba za watu binafsi. Kwa mujibu wa madereva hao, ushuru huo wa Sh15, 000 hutozwa na uongozi…