Wagonjwa wa saratani waongezeka mara sita kwa miaka 17, watoto wafikia 400 Bugando
Mwanza. Idadi ya wagonjwa wa saratani wanaotibiwa katika idara ya saratani ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando imeongezeka kutoka wagonjwa 320 mwaka 2009 hadi kufikia 2,000 kwa sasa, ikionesha ukubwa wa tatizo hilo mikoa ya Kanda ya Ziwa. Akizungumza leo Februari 15, 2026 katika maadhimisho ya Siku ya Saratani za Watoto Duniani yaliyofanyika…