Waliorejeshwa Soko Kuu Kariakoo wahofia kuyaachia maeneo walikohamishiwa

Dar es Salaam. Zile kelele za baadhi ya wafanyabiashara kutishia kuandamana baada ya majina yao kutokuwamo kwenye orodha ya wanaotakiwa kurejea Kariakoo, sasa zimegeuka shubiri kufuatia kufunguliwa rasmi kwa soko hilo. Soko la Kariakoo lilifunguliwa Februari 8, 2026 baada ya kukarabatiwa kwa miaka minne tangu lilipoungua moto na kuteketeza mali za wafanyabiashara. Tayari baadhi yao…

Read More

Wanafunzi wanne wajeruhiwa ajalini, 16 wakinusurika

Moshi. Wanafunzi 16 wa Shule ya Msingi FM Foundation iliyopo Manispaa ya Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro wamenusurika baada ya gari aina ya Toyota Hiace walilokuwa wakisafiria kupinduka na kuangukia korongoni bada ya  kukosa mwelekeo. Katika ajali hiyo, watu wanne wamejeruhiwa wakiwamo wanafunzi wawili wa shule hiyo, dereva wa gari na msaidizi wake. Majeruhi hao wamepelekwa…

Read More

Anayedaiwa kuzalisha pombe bila leseni aburutwa mahakamani

Geita. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Geita imefikisha mahakamani Mkurugenzi wa Matondo Breweries Investment Company Limited, Matondo Malanda wa Uyovu, Kata ya Buganzu, Wilaya ya Bukombe, akihojiwa kwa makosa manane ya kodi na forodha, ikiwemo uzalishaji wa pombe bila leseni inayostahili. Malanda alipandishwa kizimbani Februari 10, 2026 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, mbele…

Read More

TANZANIA YALENGA ASILIMIA 51 YA WANAWAKE KATIKA SAYANS

…………… Na Carlos Claudio, Dodoma. Serikali imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwekeza katika elimu ya sayansi ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira na kasi ya ukuaji wa teknolojia duniani, huku ikiweka mkazo maalum katika kuongeza ushiriki wa wanawake na wasichana katika sekta hiyo. Akizungumza Februari 11, 2026 jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Siku…

Read More

Familia ya Rais Edgar Lungu yapata pigo jingine

Dar es Salaam. Zikiwa zimepita siku 251 tangu kifo cha Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu huku mwili wake ukiwa bado haujazikwa, Serikali ya Zambia imemnyang’anya mwanaye Dalitso Lungu, mali zenye thamani ya Sh3.37 bilioni, yakiwamo magari 79. Lungu aliongoza Zambia kuanzia mwaka 2015 hadi 2021 aliposhindwa katika uchaguzi mkuu na Rais wa sasa,…

Read More

Rais Samia ateua wapya, yumo Anne Makinda

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi katika taasisi mbalimbali za umma, akiwemo Spika mstaafu wa Bunge, Anne Makinda. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano, Februari 11, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Moses Kusiluka na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu, imeeleza kuwa uteuzi…

Read More

Rostam: Serikali imeongeza imani ya wawekezaji nchini

Dar es Salaam. Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz amesema anaamini taasisi za Serikali zimeimarika vya kutosha na kuwapa wawekezaji imani katika kuwekeza miradi mikubwa nchini Tanzania. Amesema hata kama kunaweza kuwepo na siasa zisizotabirika, lakini sera na mifumo thabiti iliyowekwa inatosha kujenga uaminifu kwa miaka mingi zaidi. Rostam amebainisha hayo katika makala iliyochapishwa kwenye Jarida…

Read More