Wagosi wamaliza gundu la siku 76
USHINDI wa mabao 4-1 ilioupata Coastal Union mbele ya Tanzania Prisons umeiwezesha kuondoa jinamizi la siku 76 bila ushindi Ligi Kuu Bara, huku kocha Mohammed Muya akisema haikuwa rahisi kwani bado wanaijenga timu. Wagosi wa Kaya walipata ushindi mara ya mwisho miezi miwili na siku 15 walipoinyoa Mbeya City mabao 2-0 katika mechi ya Ligi…