Ukeketaji ukipungua, wadau wataka sheria kulinda wanawake watu wazima
Dar es Salaam. Wakati matukio ya ukeketaji yakitajwa kupungua hadi kufikia asilimia nane, wadau wa haki za binadamu wameitaka Serikali kutunga sheria maalum ya kupinga ukeketaji itakayowalinda pia wanawake watu wazima. Pia, wametaka kutungwa na kutekelezwa kwa sheria ndogo-ndogo katika mikoa yenye viwango vikubwa vya matukio ya ukeketaji, sambamba na kufanyiwa marekebisho Sheria ya Ndoa…