Haya hapa maagizo ya Rais Samia akizindua Soko Kuu Kariakoo
Dar es Salaam. Huenda Soko la Kariakoo unalolifahamu au kuwahi kulisikia likawa na taswira mpya, baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza utaratibu mpya wa maegesho, njia za kusafirisha mizigo na kufunguliwa kwa barabara zinazoingia na kutoka sokoni humo. Lingine aliloelekeza ni kujengwa kwa maeneo ya watoto kucheza, kuimarishwa ulinzi, viwango vya ubora wa bidhaa…