Ajali ya lori, bodaboda ilivyopoteza maisha ya watoto watatu Iringa
Iringa. Watu wanne, wakiwamo watoto watatu na dereva wa bodaboda, wamefariki dunia papo hapo mjini Iringa baada bodaboda iliyowabeba watoto hao kugongwa na lori la mizigo aina ya Faw, mali ya kampuni ya TransAfrica. Akizungumza na Mwananchi leo Juni 29, 2024, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Alfred Mbena amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo…