Rais Samia amteua bosi mpya Usalama wa Taifa

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa leo Alhamisi Julai 11, 2024.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mululi Majula Mahendeka na kusainiwa na Sharifa Nyanga, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Mombo amechukua nafasi ya Balozi Ali Idi Siwa ambaye amestaafu.

Related Posts