KUNA tabia za ndani na nje ya uwanja alizonazo winga wa kushoto Yanga, Maxi Mpia Nzengeli (24), zinazofanana na kiungo mkabaji wa Al-Ittihad ya Saudi Arabia, Ngolo Kante (33).
Nzengeli ni kama anaendana na tabia ya jina lake, ambalo kikwao ni malaika, hana mambo mengi na kitu wanachokipenda mashabiki wake ni kuchomekea awapo uwanjani.
Staa huyo ana urefu wa 1,74 m, wakati Kante raia wa Ufaransa ana urefu ni 1:6 sawa na futi 5 na inchi 6, mastaa hao ni wapole, hawapo flonti kwenye mambo mengi zaidi ya kuona ufundi mkubwa uwanjani.
Mwanaspoti linakuchambulia baadhi ya tabia zao, zinazowatofautisha na mastaa wengine ambao wana majina makubwa katika sokam pia wanafanya vitu vingi vya kuonekana nje ya uwanja.
Mastaa hao wanazingatia muda wa kufika mazoezini, kupumzika, kula, hawana visingizio na wamekuwa mfano wa kuigwa na wengine ambao wanapenda kufanya mambo kwa kujivuta.
Marafiki wa karibu wa Nzengeli, wanasema “Anapopata mapumziko na anajua ana ratiba ya kwenda kanisani, anajiandaa mapema na anapenda kuwahi pia ukiwa na ahadi naye ni vizuri ukazingatia muda ili mwende sawa”.
Ili kuthibitisha mastaa hao ustaa umewafuata wakiwa nje ya uwanja, wanajishusha, mfano mzuri kuna video ilikuwa inamuonyesha Nzengeli akiabudu moja la kanisa jijini Dar es Salaam.
Wakati Konte, aligonga vichwa vya habari, baada ya kulitumia gari alilopewa na shabiki, huku mastaa wenzake wakiona haliendani na thamani yake.
Ni kawaida kwa mastaa kuona mabadiliko katika miili yao, kama kuvaa herini, kuchora tatoo,kubadili rangi za miili yao, ila ni tofauti kwa Konte na Nzengeli ambao wananyoa kawaida na hakuna kilichobadilika kwao.
Winga wa Yanga, Denis Nkane anashuhudia tabia za Nzengeli wanapokuwa kambini ama wakati mwingine akimtembelea nyumbani kwake”Mara nyingi kambini ukimkuta chumbani kwake, anakuwa anasikiliza nyimbo za dini, kifupi hana mambo mengi.”
Nkane aliwahi kumfanyia mahojiano, akimuuliza anapenda kutoa pasi ama kufunga? Alijibu “Napenda sana kutoa asisti.”
Siyo wachezaji machepele, wagumu kuzoeana na kila mtu, mara nyingi wanapenda kujitenga na kelele, usoni kwao kumetawaliwa na aibu.
Kutokana na aibu aliyonayo Kante mwaka 2018 wakati ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa lake la Ufaransa, alikwepa kupigwa picha na wachezaji wenzake, alichofanya alijificha nyuma ya staa mwenzake Paul Pogba ambaye kabla ya kufungiwa timu ya mwisho aliyokuwa ameichezea ni Juventus.
Katika hilo kwa Nzengeli ni tofauti kidogo, picha ya pamoja na wachezaji wenzake ni rahisi kumpata, ila yapo baadhi ya matukio ambayo anakuwa mwenyewe, mfano wakati timu ya Yanga inaingia kukagua Uwanja wa Benjamin Mkapa, kabla ya kucheza fainali za Ngao ya Jamii, alikuwa mbele akiwa peke yake, huku akiwa amevalia airphone masikioni, kuna muda alikuwa anatazama nyuma kama kujishitukia, kujiona yupo mbali na wenzake.
Baadhi ya mashabiki walioshuhudiwa na Mwanaspoti, wakimsema Nzengeli kwamba hana mambo mengi ila wanafurahisha na nguvu anayoitumia uwanjani ambapo msimu wake wa kwanza Yanga alifunga mabao 11.
NDANI YA UWANJA NI HATARI
Nzengeli akiwa uwanjani, ana kasi wakati mwingine anaibia majukumu ya wengine wanapojisahau, ndivyo ilivyo kwa Kante ambaye anakuwa msaada mkubwa kwa mabeki na ana kasi.
Nzengeli ndiye aliyeivusha Yanga kutinga fainali, baada ya kuifunga Simba bao 1-0, ukiachana na hilo,kiwango alichokionyesha Afrika Kusini, Yanga ikinyakua taji la Toyota Cup, timu nyingi zilivutiwa na kiwango chake, ila ikawa ngumu kwa viongozi kumuachia.
Kante ana CV kubwa kuliko Nzengeli, kutokana na timu alizochezea na mafanikio aliyopata pia kiumri ni mkubwa.
2015–2016: Leicester City
2023– Al-Ittihad ya Saudi Alabia
2016: Bingwa Ligi Kuu England
2016: Ufaransa fainali Euro 2016
2017: Bingwa Ligi Kuu England
2017: Mchezaji Bora wa kulipwa
2017: Mchezaji bora wa Ligi Kuu
2017: Mshiriki tuzo ya Ballon d’Or
2018: Bingwa Kombe la Dunia