Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) limeiondolea adhabu ya kutosajili timu ya Fountain Gate baada ya kupata uthibitisho kuwa imelipa fidia ya mchezaji ambaye alikuwa akiidai.
Mchezaji huyo anatajwa kuwa ni Rodrigo ambaye timu hiyo iliwahi kumsajili kutoka Brazil.
Habari za uhakika kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimefichua kuwa muda wowote kuanzia sasa, taarifa rasmi juu ya uamuzi huo zitatolewa kwa umma. Kufunguliwa kwa Foutain kunaipa nafasi ya kuivaa Simba Jumapili hii, baada ya awali mechi dhidi ya Namungo kuahirishwa.
Soma zaidi kwa kutembelea www.mwanaspoti.co.tz