TUME YAVIASA VYAMA VYA SIASA KUTOINGILIA MCHAKATO WA UBORESHAJI WA DAFTARI

 

Mwenyekiti
Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele,
akizungumza wakati akifungua mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi
uliofanyika leo Agosti 25, 2024 mkoani Mara.
Wadau hao ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa,
Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya
habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi
wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa
Kimila.

Sehemu ya washiriki wa mkutano wa siku moja wa Tume
na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Agosti 25, 2024 mkoani Mara. Wadau hao ni
pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi
za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari
wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu
wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila. 

Sehemu ya washiriki wa mkutano wa siku moja wa Tume
na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Agosti 25, 2024 mkoani Mara. Wadau hao ni
pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi
za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari
wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu
wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila. 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akizungumza wakati akiwasisha mada ya maandalizi ya uboreshaji kwa wadau wa uchaguzi Mkoa wa Mara. 

Mkurugenzi wa Daftari na TEHAMA wa Tume Huru ya
Taifa ya Uchaguzi, Stanslaus Mwita akiwasilisha mada ya mifumo wakati wa
mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Agosti 25,
2024 mkoani Mara.

Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
(INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akiteta jambo na Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa Tume, Bw. Kailima Ramadhani wakati wa mkutano wa siku moja wa Tume
na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Agosti 25, 2024 mkoani Mara.

Wadau wakishiriki katika majadiliano. 

Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akiongoza majadiliano. 

Wadau wa uchaguzi wakiwa katika majadiliano.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Bw. Kailima Ramadhani akijibu hoja mbalimbali wakati wa mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Agosti 25, 2024 mkoani Mara.

***************

Na. Waandishi wetu, Mara
Tume Huru ya
Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeviasa vyama vya siasa kutoingilia mchakato wa
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika vituo vya kuandikishia
wapiga kura.
 
Wito huo
umetolewa leo tarehe 25 Agosti, 2024 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jacobs Mwambegele, wakati akifungua
mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika mkoani Mara.
 
Mhe. Jaji
Mwambegele amesema mawakala au viongozi wa vyama vya siasa hawaruhusiwi
kuingilia mchakato wa uboreshaji vituoni kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume
na sheria ya uchaguzi.
 
Amehimiza
viongozi wa vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuzingatia sheria ya uchaguzi,
kanuni za uboreshaji, maelekezo ya tume, na kusimamia miiko na mipaka ya
uendeshaji wa zoezi la uboreshaji wa Daftari.
 
Pia
amevitaka vyama vya siasa kutumia sheria zilizopo kuwasilisha changamoto
zinazojitokeza kwa tume, ambapo ameongeza kuwa INEC itazingatia Katiba, sheria
ya uchaguzi, na kanuni zilizotungwa chini ya sheria katika zoezi la uboreshaji.
 
Akiwasilisha
mada kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya
Uchaguzi, Bw. Ramadhan Kailima amsema Tume inategemea vyama vyenye usajili
kamili kutumia fursa za kisheria zilizotolewa kwao kuhakikisha zoezi la
uboreshaji linafanikiwa na kuongeza kuwa endapo kutajitokeza changamoto zozote
wakati wa zoezi, Vyama vitumie taratibu zilizoainishwa kwenye sheria
kuwasilisha changamoto hizo.
 
“Viongozi wa
vyama hawapaswi kuingilia utekelezaji wa majukumu ya watendaji wa vituo wakati
wote wa uandikishaji wa wapiga kura vituoni kama kuomba orodha au idadi ya
walioandikishwa au kuboresha au kuhamisha taarifa zao,”
 
Ameeleza
kuwa, Tume inaowajibu wa kuwapatia vyama vya siasa taarifa hizo mara baada ya
zoezi kukamilika.
 
Mkutano kama
huo umefanyika pia mkoani Simiyu na Manyara ambapo akifungua mkutano mjini
Bariadi, mkoani Simiyu, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,
Mhe. Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk S. Mbarouk, amewataka wadau
kuwaelimisha wananchi kujiandikisha mara moja tu ili kuepuka uvunjaji wa
sheria.
Naye Mjumbe
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari,
ambaye alifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Manyara, amewahimiza watu
wenye ulemavu, wazee, wagonjwa, wajawazito, na akina mama wenye watoto wachanga
watakaokwenda nao vituoni kujitokeza kwa wingi kwa kuwa watapewa fursa ya
kuhudumiwa bila kupanga foleni.
 
Mikutano
hiyo ni maandalizi ya mzunguko wa nne wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura ambao utajumuisha mkoa wa Mara, Simiyu na  baadhi ya halmashauri za Mkoa wa Manyara
ambazo ni Halmashauri ya Mji wa Babati na Halmashauri za Wilaya za Babati,
Hanang na Mbulu ambapo uboreshaji utaanza tarehe 04 Septemba, 2024 hadi 10
Septemba, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na
kufungwa saa 12:00 jioni.

Related Posts